Habari za hivi Punde

TUME YA UCHAGUZI IMEKUJA NA MFUMO MPYA WA UANDIKSHWAJI MAJINA KWAAJILI YA KUPIGA KURA.Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Damian Lubuva  akifungua  semina kwa waandishi wa habari mkoani Shinyanga ambapo alieleza kuwa  kwa niaba ya tume ya taifa ya uchaguzi, sasa kuna maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura   ambapo zoezi la uandikishwaji utaanza hivi karibuni. Anasema kwa awamu ya kwanza  watatumia mfumo mpya wa teknolojia  ya BIOMETRIC VOTER REGSTRATIO (BVR)  ambao ni mfumo wa kuchukua  au kupima  taarifa za mtu za kibaiolojia au tabia ya mwanadamu na kuzihifadhi katika kanzi data kwa njia ya utambuzi,mfumo huo pia hutumika katika kumtambua mtu na kumtofautisha  na mwingine.
 

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakisikiliza kwa makini taarifa hiyo kutoka kwenye tume ya uchaguzi huku wakieleza kuwa muda wa siku 14 uliotengwa hautoshi  kwa wananchi kujiandikisha hiyo itakuwa changamoto hasa kwa kuangalia mazingira ya nchi yetu na jiografia yake miundombinu mibovu sanjari na msimu wa kilimo kuanza  wananchi watashindwa kwenda kujiandikisha  kwa muda huo hivyo walimshauri mwenyekiti wa tume kuweza kuangali suala la muda wa kujiandikisha.


Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini  taarifa iliyokuwa ikitolewa na  wawakilishi wa tume ya uchaguzi taifa .


Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi taifa Damian Lubuva akiandika hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na waandishi wa habari ambao hawapo pichani.


Afisa elimu mpiga kura taifa  Salvatory Alute akieleza historia fupi ya daftari la kudumu la wapiga kura ambalo  mchakato  wa kuanzishwa kwakwe ulikuwa mwaka 2004 ambapo ulienda sambamba  na matumizi  ya teknoloji  ya ukusanyaji taarifa  za wapiga kura  pamoja na uhifadhi wa taarifa hizi kielektroniki hicho anasema kuwa changamoto iliyojitokeza  kwenye daftari hilo ni baadhi ya watu kukosa majina,viongozi wa vijiji na kata kutopeleka taarifa ya waliofariki hivyo tume imeona kuna umuhimu wa kufanya maboresha  upya na itatoa kadi tofauti na zilizvyokuwa awali  na kutumika kama ilivyokuwa  mwanzo  mpaka pale vitakapo patikana vitambulisho vya taifa.
Mwandishi wa habari gazeti la jamboleo Steven Kidoyai akitoa hoja ya kwanini  mtu hawezi kupiga kura akiwa kwenye eneo tofauti na alipojiandikishia kwani inaonekana kumyima haki mtanzania kupiga kura isitoshe wengine ni wafanyabishara mara nyingi husafiri.
Baada ya kukamilisha semina hiyo fupi kwa waandishi wa habari mwenyekiti aliwashukuru waandishi hao na kuwataka waweze kusambaza habari hizi katika maeneo yote ili wananchi waweze kufikiwa na taarifa za tume,huku akieleza kuwa kumekuwepo na changamoto ya kusema kuwa tume inapendelea chama fulani sio kweli ingawa viongozi wake wanateuliwa na Rais haiwazuii kufanya kazi kwa kuwa huru.

KARENY. Powered by Blogger.