WAZIRI
wa sheria na katiba wa serikali ya wanafunzi kutoka chuo cha usimamizi
wa fedha IFM kilichopo jijini Dar es salaam Kasanzu Luganga ambaye yuko
Shinyanga kwa ajili ya kufanya mazoezi kwa vitendo ofisi ya bima ya afya
(NHIF),akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga ,ambapo
alisema tangu
waanze mazoezi kwa vitendo miezi miwili imepita hakuna fedha iliyotumwa
na
serikali kwa ajili ya kujikimu wakati wa (Field) hali ambayo
imesababisha waishi katika mazingira magumu kwa kuomba omba fedha kwa
ndugu,jamaa na marafiki ili waweze kujikimu kimaisha. Alisema kuchelewa kwa fedha za kujikimu wanafunzi wa vyuo
vikuu ambao wako katika mazoezi ya vitendo mkoani Shinyanga,kumesababisha baadhi
yao kugeuka kuwa ombaomba kutokana na
kukosa fedha za kulipia kodi za nyumba walizopanga na huduma zingine muhimu
ikiwa ni pamoja na kununu chakula na matibabu na ameitaka serikali kutoa fedha hizo sh 620,000 kwa mwezi ili kuwaondolea kero.
| | |
|
0 Response to "WANAFUNZI VYUO VIKUU WADAIWA KUWA OMBAOMBA MITAANI."
Post a Comment