MADIWANI wa Halmashauri ya wilaya ya Meatu Mkoani
Simiyu wamewafuta kazi watendaji watano wa serikali za vijiji na mmoja mtendaji wa kata kwa kile kilichodaiwa utoro kazini bila kutoa taarifa pamoja na kuzarau viongozi
wa ngazi za juu ndani ya Halmshauri hiyo.
Akitoa azimio la Madiwani katika
kikao cha Baraza la halmashauri kilichofanyika katika ukumbi wa Halmshauri hiyo Mwenyekiti wa
baraza hilo Pius Machungwa alisema madiwani wameazimia kuwafukuza kazi
watumishi hao.
Machungwa alisema kuwa kutokuwepo
kwa watendaji hao kwa muda mrefu katika maeneo yao ya kazi imesababisha
wananchi kushindwa kuhudumiwa ipasavyo hasa kutatua kero mbalimbali
zinazowakabili ndani ya vijiji vyao.
“wamekuwa watoro kwa kipindi
kirefu..lakini pia tulishawandikia barua za onyo ili kuweza kujirekebisha
wamepuuza barua zetu na za waajiri wao hivyo baraza la madiwani limeamua
kuwafuta kazi watumishi hawa kwa makosa hayo”
Alibainisha kuwa Katika vijiji
walivyokuwa watendaji hao kulionekana miradi ya maendeleo kusimama kwa muda
mrefu bila ya kuendelezwa kutokana na kukosekana kwa usimamizi wao hali
iliyosababisha miradi hiyo kutelekezwa na makandarasi.
Waliofukuzwa kazi ni pamoja na Shiwa
Charles ambaye ni mtendaji wa kata ya Bukumbi,Paul Lalida mtendaji wa kijiji
cha Nata,John Joseph mtendaji wa kijiji cha Baluli na Richard Matanga ambaye ni
mtendaji wa kijiji cha Witamhinya.
Mwingine ni Charles Makaranga ambaye
ni mtendaji wa kijiji cha Mwaga huku Halmashauri hiyo ikimpa onyo kali Afisa
ugavi msaidizi Emanuel Marwa kwa kosa la kudharau viongozi wa ngazi za
juu pamoja na watumishi wenzake.
Katika hatua nyingine mwenyekiti
huyo amewataka watendaji wa vijiji na kata kusimamia kesi za migogoro ya mipaka
ya shule za msingi na sekondari ili kuweza kuhakikisha maeneo yenye migogoro
yanatatuliwa.
|
0 Response to "WAZIRI HAWA GHASIA KULIKONI KWA WATUMISHI HAWA WA SERKALI ZA VIJIJI WILAYANI MEATU?"
Post a Comment