Mbunge
wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete akiongozana na akina mama wa
jamii ya kimasai waliobeba maji waliyoyateka baada ya mbunge huyo
kuzindua kisima cha maji katika Kijiji cha Mbala, Chalinze, Bagamoyo
mkoani Pwani jana. Kisima hicho pamoja na lambo la kunyweshea mifugo
vimejengwa na Kanisa la Wasabato kwa gharama ya sh. mil. 76. Kushoto ni
Kiongozi wa mradi huo, Joseph Chagama na nyuma yake ni Askofu wa Kanisa
la Wasabato Jimbo la Mashariki,Mark Malekana. (PICHA NA RICHARD
MWAIKENDA)
Ridhiwani
Kikwete akifunua pazia ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima hicho.
Kushoto ni Askofu wa Kanisa la Wasabato Jimbo la Mashariki,Mark
Malekana.
Ridhiwani akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa jamii ya kimasai baada ya kuzindua kisima hicho.
Mama mwingine wa Jamii ya Kimasai akitwisha ndoo ya maji na Ridhiwani Kikwete
Ridhiwani
Kikwete akifungua maji ikiwa ni ishara ya kuzindua lambo la kunyweshea
mifugo katika Kijiji cha Mbala kinachokaliwa kwa asilimia kubwa na jamii
ya wafugaji
Ng'ombe wakitoka kunywa maji kwenye lambo hilo
0 Response to " WANANCHI WA JAMII YA WAFUGAJI KIJIJI CHA MBALA CHALINZE WAPATA UHAI."
Post a Comment