Habari za hivi Punde

SEKTA YA AFYA MUONENI MWANAMKE MARTHA, UZAZI WA MPANGO KWAKE NI NDOTO

Mwanamke  Martha Martin  anayeishi katika kitongoji  cha mocha kijiji cha kakola kata ya Mwenge halmashauri ya wilaya ya Shinyanga  akiwa na wanawe  watano  katika historia  yake anasema kuwa  hajawahi kwenda shule anaendesha maisha yake kwa kufanya vibarua ,hafahamu  juu ya elimu ya uzazi wa mpango pia watoto wake wote amezalia nyumbani ambapo katika picha hiyo anayedaiwa ni mkubwa wao hana tofauti na wale wadogo,mwanamke huyo anaeleza kuwa hata wakiugua mara nyingi  amekuwa akitumia miti shamba kutokana na ugumu wa   kupata fedha ,hivyo  hata mlo wa siku umekuwa ni shida kwake katika hali hiyo anaishi na mzazi mwenzake ambaye hujishughulisha na udreva wa daladala  ya baiskeli mjini mara nyingi amekuwa haonekani nyumbani  wakati mwingine siku tatu zinapita.

Mwanamke Martha  Martin akiwa nyumbani kwake na wanaye ambao hata hao watoto hawasomi,ikiwa naye hajui kusoma wala kuandika anaeleza kuwa huduma ya kupata matibabu ni mbali hivyo hushindwa kuendea  dawa hata  alizonazo mzazi mwenzie humletea kutoka mjini tena bila ya mtoto kupimwa na kufahamu anasumbulia na tatizo gani, ambapo wataalamu wanaeleza kuwa chanzo cha upungufu wa damu kwa mtoto ni kuugua malaria kwa muda mrefu bila kutibiwa,lishe duni, lakini  familia hii  kumekuwa na changamoto kubwa na  imekuwa na mazoea kunywa dawa bila kupimwa na daktari hata utumiaji wa chandarua hakuna.

Mtoto huyu anakadiriwa kuwa na miezi saba,  anaumwa ila ugonjwa wenyewe  haujathibitishwa na dakitari,hata kuzaliwa kwake alizaliwa nyumbani,ikiwa Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe alisema kuwa idadi ya mama wanaojifungilia majumbani ni asilimia 30 hadi 40  jambo ambalo ni hatari pia ili kupata vipimo sahihi kwa ugonjwa unaosumbua lazimia kuonana na daktari  ,upungufu wa damu unaletwa na kutotibu ugonjwa unaokusumbua kwa muda mrefu hasa malaria,lishe duni ambayo inafanya watoto kuwa wadumavu ikiwemo mama kutofuata uzazi wa mpango.

0 Response to "SEKTA YA AFYA MUONENI MWANAMKE MARTHA, UZAZI WA MPANGO KWAKE NI NDOTO"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.