Kijana
anayejitambulisha kwa jina la Robert Lugala, anayedai kutishiwa maisha
na Mchungaji Lusekelo Anthon. Akizungumza na waandishi wetu juzi jijini
Dar, Robert ambaye shughuli zake ni kuuza chipsi usiku kucha, alisema
mara kwa mara Mzee wa Upako amekuwa akimfuata eneo lake la kazi na
kumtishia maisha kwa kumwambia maneno mbalimbali yenye vitisho.
“Mara ya kwanza ilikuwa Oktoba 9, mwaka huu saa kumi kasoro usiku. Alipaki gari lake, Land Cruiser (Toyota) nyeusi.
LILE
sakata la Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo – Kibangu, Dar,
Lusekelo Anthon ‘Mzee wa Upako’ kufyatua risasi mtaani limechukua sura
mpya baada ya kijana aliyejitambulisha kwa jina la Robert Lugala, mkazi
wa Kibangu kuibuka na kudai alitishiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na
mchungaji huyo
Akaniangalia
na kuniambia nina macho makali. Akasema ataniombea nitaanguka.
Nikamkatalia na kumwambia mimi nina nguvu za Mungu wa kweli, nasali kwa
Gwajima kwa hiyo siwezi kuanguka. Aliposhindwa akaahidi kurejea siku
nyingine.
“Mara ya
pili ni Oktoba 13, mwaka huu saa nne usiku alikuja tena. Mara ya tatu ni
Oktoba 15 saa kumi usiku akaanza kugawa pesa kwa madereva wa bodaboda
huku akiwaamrisha kuniimbia nyimbo ya kunilaani. Kweli waliniimbia.
0 Response to "ATHONY LUSEKELO (MZEE WA UPAKO) ADAIWA KUMTISHIA MAISHA KIJANA AMBAYE NI MUUMINI WA GWAJIMA."
Post a Comment