Habari za hivi Punde

SERIKALI YA CHINA IMELAANI VIKALI KUHUSISHWA TUHUMA ZA NDEGE YA RAIS KUBEBA MENO YA NDOVU

Balozi wa China nchini Tanzania,Mh. Lu Youqing akizungumza na vyombo vya habari mjini Arusha leo juu ya tuhuma za kuhusishwa kwa Ndege ya Rais wa China kubeba meno ya ndovu kutoka nchini.Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Lazaro Nyalandu na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii,Mh. James Lembeli.
Serikali ya China imelaani vikali uzushi uliotolewa na vyombo vya magharibi kutuhumu ndege ya Rais huyo kutumika kubeba meno ya ndovu kutoka nchini.

Akizungumza leo mjini Arusha Balozi wa China Lu Youqing alisema kuwa huo ni uongo mkubwa ambao ulikuwa na nia ya kutia aibu taifa lake na Tanzania kwa ujumla.

Alisema kwamba Taifa lake hutoa adhabu kali kwa mtu anayefanya uovu kama ujangili, "Kama mwandishi angeweza kuthibitisha hao maafisa wangechukuliwa hatua kali, na hilo liko ndani ya uwezo wangu kwanini ameshindwa kuwataja?"

Lu alisema kwamba Adhabu kama hiyo si kwa mtu aliyekutwa na nyara tu bali hata kwa muongo, "Mwandishi huyo ni muongo na anatakiwa aadhibiwe".

Waziri wa maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu aliunga mkono kauli hiyo na kusema kuwa ilikuwa na nia ya kuchafua hali ya hewa kutokana na mkutano wa kimataifa ulioanza leo jijini Arusha.

"Hata tulipokwenda na rais Kikwete jijini London kwa mkutano wa kimataifa juu ya ujangili gazeti la Dail Mail lilitoa habari za kashfa kuhusu Tanzania siku moja kabla ya mkutano na hii leo ndio limetokea"

Alisema nashukuru wadau wa uhifadhi ambao kwa kiwango kikubwa wamehudhuria kikao chetu muhimu cha leo ambacho kitaleta mabadiliko makubwa katika vita dhidi ya ujangili.

Kikao hichio kilihudhuriwa na mawaziri kutoka nchi tisa za Afrika ukanda wa bahari ya Hindi na afrika mashariki na Kati pamoja na wawakilishi wa mashirika mbalimbali na balozi wa nchi nyingi wanaowakilisha nchi zao.

0 Response to "SERIKALI YA CHINA IMELAANI VIKALI KUHUSISHWA TUHUMA ZA NDEGE YA RAIS KUBEBA MENO YA NDOVU"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.