WAUMINI wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania-KKKT-mission
ya Tabora wametakiwa kuisoma rasimu ya katiba iliyopendekezwa na kuielewa
ili waweze kuipigia kura ya maoni.
Akizungumza katika ibada ya Jumapili Mchungaji Kiongozi wa Kanisa
la KKKT mission ya Tabora, Patrick Kiula, alisema waumini wamekuwa ni watu
wavivu wa kusoma na hivyo kubaki kulalamika tu.
Kiula alisema waumini wanatakiwa kushiriki kikamilifu katika
masuala ya jamii ikiwemo katika kuisoma rasimu ya katiba na kuipigia kura ili
kuweza kuwa na katiba inayowajali Watanzania.
Alisema kwa sasa rasimu ya katiba iliyopendekezwa inapatikana
hivyo kinachotakiwa ni waumini kuitafuta kwa hali na mali na kuisoma ili kuweza
kutambua vitu vilivyopendekezwa kwenye rasimu hiyo.
Mchungaji KIULA aliwataka waumini hao kuacha tabia ya uvivu wa
kujisomea vitu vya msingi hasa vya kijamii ili kuhakikisha kuwa wanakwenda
sambamba na watu wengine kuliko kukaa bila kufahamu kinachoendelea katika
nchi yao.
0 Response to "WAUMINI WA KANISA LA KKKT WAMETAKIWA KUISOMA KATIBA PENDEKEZO."
Post a Comment