Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa
wilaya ya Kahama Benson
Mpesya kwenye maafali ya kumaliza kidato cha nne kwa wanafunzi wa shule ya
sekondari ya Kishimba iliyopo katika halmashauri ya mji wa Kahama.
Katika mahafali hayo Mpesya aliyewakilishwa na Afisa uhamiaji
wilayani humo Zacharia Misana alisema ili kupata ajira ni kusoma masomo ya
sayansi yatakayoweza kuwapa ujuzi wa kupata maarifa ya kujiajiri wenyewe badala
ya kutegemea ajira.
Mkuu wa shule hiyo Melkisedeck Choya alisema usomaji wa masomo ya
sayansi katika shule hiyo ni mgumu kutokana na kuwa na maabara ambayo
haijakamilika pamoja na serikali kufanya jitihada za kuyakamilisha kwa haraka.
Choya alisema pamoja na changamoto hiyo shule ya sekondari
Kishimba, ilikuwa ikikabiliwa na uporomokaji mkubwa wa maadili, na kwamba hivi
sasa jitihada za kuirudisha kwenye nidhamu zinaendelea kwa ushirikiano wa
walimu, wazazi na jamii inayowazunguka.
Katika mahafali hayo jumla ya shilingi milioni moja na nusu
zimechangwa na wazazi waliokuwa wamehudhutia pamoja na mifuko 19 ya saruji
iliyotolewa na walimu wa shule hiyo, ili kukabiliana na tatizo la maabara
zisizokamilika.
0 Response to "WANAFUNZI WAASWA KUSOMA MASOMO YENYE TIJA YANAYOENDANA NA SOKO LA AJIRA."
Post a Comment