|
Maelfu
ya wakazi wa mji wa Shinyanga na maeneo ya jirani waliojitokeza jioni
ya leo katika viwanja vya mahakama ya mwanzo Nguzo nane mjini Shinyanga
katika mkutano mkubwa wa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa
ndugu Halima Mdee ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kawe.Pamoja na mambo
mengine viongozi mbalimbali wa Chama hicho walisisitiza umuhimu wa
kujiandikisha katika daftari la wapiga kura na kujitokeza kupiga kura
katika uchaguzi wa serikali za mitaa Desemba 14,2014 huku wananchi
wakishauriwa kuachana na propaganda za CCM ambayo imeshindwa kuwaondoa
Watanzania katika umaskini,kila siku maisha yanazidi kuwa magumu-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Viongozi mbalimbali wa Chadema ngazi ya wilaya,mkoa na taifa wakiwa jukwaa kuu jioni ya leo mjini Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
|
Mwenyekiti
wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga mjini Hassan Baruti akifungua mkutano
leo mjini Shinyanga ambapo aliwaomba wananchi kuungana kwa pamoja ili
kuing'oa CCM madarakani na kuwapuuza wanaohama chama kwani wanatumiwa na
watu wasioitakia mema Chadema-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
Mak
|
Mwenyekiti
wa Chadema mkoa wa Shinyanga Peter Machanga akiwasalimia wananchi wa
Shinyanga huku akiwataka wakurugenzi wa wilaya kutoa vipeperushi kuhusu
taratibu za uchaguzi wa serikali za mitaa-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Wananchi wakinyoosha mikono kufurahia hotuba za viongozi wa Chadema jioni ya leo-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
|
Mbunge wa Maswa Mashariki Sylivester Kasulumbayi akiongea na wananchi wa Shinyanga leo-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
Maelfu ya wananchi wakifuatilia mkutano wa Chadema jioni leo mjini Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
|
Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Shinyanga pia mwenyekiti wa baraza la wanawake
Chadema mkoa wa Shinyanga,Rachel Mashishanga akikaribisha wageni wa
kitaifa wakiongozwa na mwenyekiti wa BAWACHA taifa Halima
Mdee.Mashishanga alisema pamoja na serikali kuwapa wakazi wa Shinyanga
Waziri wa madini,Stephen Masele lakini mbunge huyo hana msaada wowote
kwa wananchi huku akiwataka watu wa Shinyanga kubadilika na kuiunga
mkono Chadema-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
Wakazi wa Shinyanga wakifuatilia mkutano wa Halima Mdee jioni ya leo-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
|
Naibu
katibu mkuu BAWACHA taifa Kunti Yusuph aliwasalimia wakazi wa Shinyanga
ambapo aliwataka kuungana na Chadema ili kutengeneza maisha ya sasa na
ya vizazi vijavyo-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
Mkutano unaendelea-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Katibu
mkuu BAWACHA taifa Grace Tendega akizungumza na wakazi wa Shinyanga
ambapo alisema viongozi wengi wa CCM wanajinufaisha wao na watoto wao
huku watanzania wakiendelea kuteseka na maisha magumu.Alisem njia pekee
ya kuiondoa CCM ni kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la
wapiga kura na kupigia kura viongozi wa vyama vya upinzani.Lakini pia
aliwakumbusha umuhimu wa kulinda kura zao ili zisiibiwe kama
ilivyofanyika chaguzi zilizopita kwani hata mbunge wa Shinyanga Stephen
Masele aliiba kura akashinda hivyo sasa wawe makini-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Wananchi wakifuatilia mkutano-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Makamu
mwenyekiti BAWACHA taifa Hawa Waipunga akizungumza mjini Shinyanga
ambapo aliwataka wananchi kuunga mkono kiongozi yeyote kutoka vyama vya
upinzani (UKAWA) anayeonekana kukubalika katika jamii ili kuiondoa
madarakani CCM-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Mjumbe
wa kamati kuu ya Chadema,pia mwenyekiti wa Bawacha mkoa wa Kilimanjaro
pia mbunge wa viti maalum Chadema mkoa wa Kilimanjaro Grace Kiwelu
akiwasalimia wakazi wa Shinyanga ambapo aliwataka wananchi kuendelea
kuiunga mkono Chadema na UKAWA lakini akawakumbusha kuchangia chama
hicho-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
|
Mwenyekiti
wa BAWACHA taifa Halima Mdee akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapoa
alisema kitendo cha CCM kuchakachua kura ulitokana na wananchi kutolinda
kura zao na sasa wamejipanga vyema ili kuhakikisha kuwa wanaingia ikulu
huku akilitaka jeshi la polisi kukaa pembeni ili waishughulikie
ipasavyo CCM kwani imechoka na nchi imeuzwa imebaki listi tu.Mdee
alitumia fursa hiyo kuwataka wasukuma/watu wa kanda ya ziwa ambao wapo
zaidi ya milioni 8 kubadilika kwani wana utajiri wa kila aina ikiwemo
migodi 7 mikubwa lakini ni maskini kutokana na kukumbatia serikali
isiyojali wananchi wake-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
|
Mwenyekiti
wa BAWACHA Halima Mdee akiwapokea wazee wawili walioamua kuokoka na
kurudi Chadema kwa kile walichodai CCM kutojali wananchi.Mwenye shati la
kitenge ni mzee Joseph Rweyemamu(58) aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji cha
Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga kwa muda wa miaka 15,akifuatiwa
na mzee Robert Ng'welo(66) aliyekuwa katibu mwenezi wa CCK mtaa wa
Jikolile kata yaNdembezi-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
Mzee
Robert Ng'welo akikabidhi kadi ya CCM kwa HaliamMdee na kupewa kadi ya
CHADEMA jioni ya leo.Mdee alisema Chadema ni chama cha watanzania bila
kujali huyu ni mzee au la!!-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
0 Response to "MKUTANO WA CHADEMA MKOANI SHINYANGA WAHIMIZA WANANCHI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUPIGIA KURA"
Post a Comment