UKATILI wa kijinsia
katika jamii na familia
unaletwa na mtazamo hasi kwani
matendo kati ya mwanamke na mwanaume
yanategemeana ambapo mifarakano hutokea kwa kupingana na kuendeleza
changamoto zilizomo kwenye mila na desturi
ikiwemo kuwazuia watoto wa kike
kupata elimu ,ndoa za utotoni
pamoja na ukeketwaji.
Hayo yalisemwa na mwezeshaji
ambaye ni pia ni mhariri mtendaji wa gazeti la jamhuri Deogratius Balile kwenye semina
iliyowajumuisha waandishi wa habari
kutoka mikoa ya Simiyu na Shinyanga yaliyoandaliwa na chama cha
waandishi wa habari wanawake Tanzania (Tamwa) huku akieleza kuwa waandishi wananafasi kubwa ya kuibadilisha jamii .
Balile alisema kuwa ukatili wa kijinsia unaletwa kwa mtazamo
hasi ikiwa matendo kati ya mwanaume na mwanamke yanategemeana hata katika uleaji watoto katika
familia,hivyo waandishi wa habari hawana budi kuibadilisha jamii kwa kutumia kalamu zao na jinsi matukio na elimu inavyotolewa ndio jamii imeanza
kupunguza vitendo vya ukatili hapa nchini.
Alisema kwa hivi sasa
wanawake wenye umri wa kuanzia miaka 15
hadi 35 takwimu zinaonyesha kuwa ni
asilimia 39 waliokeketwa tayari huku
wenye umri wa miaka 17 hadi 24 takwimu hizo zinaonyesha pia waliokeketwa
ni asilimia 10 inaonekana kadri waandishi
wa habari wanavyoripoti elimu ya kupinga
ukatili wa kijinsia kupitia vyombo vya
habari jamii imeanza kuelewa na matukio
yamepungua.
Pia aliwataka kuondoa
dhana ya uandishi wa kiubaguzi kwa
kumtenganisha mtoto na mama katika matukio yanaporipotiwa kwenye vyombo vya
habari tofauti na wanavyoripoti matukio kwa wanaume ambapo kumejitokeza dosari ndogondogo nyingi zinazo
onyesha kumtenga mwanamke asionekane ana
haki ya kuwa katika nafasi mbalimbali au
hata katika jambo lolote linapotokea.
“Waandishi wa habari mmekuwa mkiripoti matukio
yanayotokea kwa kumtenga mtoto na mama
huku mkiwataja jinsia zao halafu majina yao yanafuata tofauti na wanaume
hawatajwi jinsia zao matokeao yake hutajwa majina hilo
nalo limeonekana ni dosari kubwa katika uripotiwaji wake nakuona kama wanawake
na watoto bado hawatendewi haki kwenye
vyombo vya habari”alisema Balile.
Balile akizungumzia suala la
kutailiwa kwa wanaume ambapo
alidai linaingizwa katika ukatili wa
kijinsia ingawa kwa hivi sasa serikali
kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii imeliunga mkono suala hilo kwa kuona
linauwezo wa kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi katika jamii.
Aliwaeleza waandishi hao kuwa kitu cha kufanya sasa ni
kusoma ili kuweza kujikomboa kiuchumi na
kuripoti vizuri matukio
yanayoendelea kutokea kwa kuyapambanua
kwa kina
jinsi ukatili unavyofanywa katika jamii
na kuondoa dosari zinazojitokeza
pindi zinaporipotiwa kwenye vyombo vya
habari .
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria semina hiyo
akiwemo selemani Abeid na Zulfa Mfinanga
walieleza kuwa ukatili bado unafanywa
katika jamii japo umepungua hivyo kupitia mafunzo hayo watatekeleza kuziondoa
dosari zilizoelezwa wakati wa kuziripoti
huku wakitaka mafunzo hayo yatolewe mara kwa mara kwa waandishi ili uelewa uwepo
zaidi.
0 Response to "UKATILI WA KIJINSIA KATIKA JAMII UNALETWA NA MTAZAMO HASI"
Post a Comment