Habari za hivi Punde

MAMA NA MWANAYE WAULIWA KIKATILI NA WATU WASIOJULIKANA
MAMA na mwanaye  wameuwawa kikatili kwa kucharangwa mapanga na watu wasiojulikana kwa kuwavamia nyumani kwao  majira ya  usiku  huko  katika kijiji cha Ngokolo wilayani Kahama mkoani Shinyanga

 Watu hao  waliofahamika kwa majina  ya Helena Charles(30)   na Mlu Nambo ( 50) 

Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga  Evarist Mangala tukio hilo limetokea juzi majira ya saa moja na nusu usiku katika kijiji hicho  wakati wakijiandaa kupata chakula cha uskiku nyumbani hapo.


Kamanda Mangala alisema siku ya tukio  marehemu Hellen na mama yake  wakiwa wanaandaa chakula cha usiku nyumbani kwao walivamiwa na watu wasiojulikana kisha kuwakata mapanga sehemu za kichwani na kisogoni ambapo walivuja damu kwa wingi na kufariki papo hapo.

Aidha  kamanda alisema chanzo cha mauaji hayo bado kinachunguzwa na tayari mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi kwa hatua zaidi za kisheria na juhudi za kuwabaini na kuwasaka wengine waliohusika na mauaji hayo bado zinaendelea.

Kamanda huyo wa polisi alitoa wito kwa wananchi kutoa  ushirikiano kwa kutoa taarifa za siri zitakazowezesha kukamatwa kwa wahusika wa mauaji hayo ili sheria iweze kuchukua mkondo wake na kukomesha mauaji kwa watu wasio hatia.

Hata hivyo  Pamoja na wanaharakati mbalimbali wa haki za binadamu kikiwemo chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) kuendelea kupinga ukatili wa kijinsia lakini vitendo hivyo vimeendela kujitokeza  ndani ya jamii.
KARENY. Powered by Blogger.