WANANCHI mkoani
Simiyu wamelilamikia Shirika la Ugavi Umeme (TANESCO) kwa tabia ya
kukata kata umeme bila taarifa na kuwaweka gizani wateja wake kwa mara kwa mara
hali ambayo inawatia hasara kubwa kwa kuunguza vyombo mbalimbali vinavyotumia
umeme ikiwemo wajasiriamali kushuka kwa vipato vyao.
Licha ya shirika hilo kuahidi mara kadhaa kuondwa tatizo la umeme linaondolewa tangu mwishoni mwa mwaka jana lakini hali ya katakata umeme na wananchi kulala gizani na kushindwa kufanya kazi za kila siku zikiwemo za ujasilia mali limekuwa kero kubwa sana kwao.
Licha ya shirika hilo kuahidi mara kadhaa kuondwa tatizo la umeme linaondolewa tangu mwishoni mwa mwaka jana lakini hali ya katakata umeme na wananchi kulala gizani na kushindwa kufanya kazi za kila siku zikiwemo za ujasilia mali limekuwa kero kubwa sana kwao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa maeneo ya miji ya Mwanhuzi,Mwandoya wilayani Meatu,Sanga mwalugesha, Lalago,Maswa mjini na Malampaka wamedai kukerwa na tabia hiyo na kuutaka uongozi wa juu wa shirika hilo kuingilia kati mwendeneo mzima wa utoaji huduma za wateja wake katika maeneo hayo.
Mohamed Shaaban mkazi wa kitongoji cha Majengo mjini Mwanhuzi alisema tabia ya kukata kata umeme bila taarifa kupitia vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikisika katika maeneo yao kumekuwa ni kero kubwa kwao na kuwasabsbishia usumbufu mkubwa hasa wajasilia mali wanotegemea nishati hiyo.
Mwalu Shigela mkazi wa Mwandoya tarafa ya Kisesa wilayani Meatu ambaye ni mjasilia mali wa biashara ya kuchomelea vyuma alisema kuwa kwa siku tatu mfululizo amekumbwa na kero ya umeme na kusababisha ugomvi kati yake na wateja walimletea zabuni ya kuchomelea madirisha na mageti ya
nyumba zao.
Naye Juma Masanja mkazi wa kijiji cha SangaMwalugesha ambaye huuza vinywaji baridi amelitupia lawama shirika hilo kwa kuonyesha uzembe mkubwa wa kuondoa nguzo zilizo oza kilio ambacho wanadai walikiwasilisha tangu mwaka juzi baada ya njia hiyo kuwa ya muda mrefu.
Wakizngumza kwa sharti la kutotajwa majina baadhi ya wakazi wa mji mdogo wa Maswa wamedai kuwa imekuwa ni tabia ya TANESCO kuzima umeme jinsi inavyotaka na imekuwa na tabia ya kurejesha umeme aidha usiku na kukata asubuhi au kutwa mzima na wafanyabaishara kuathirika na hali hiyo.
Alipohojiwa juu ya hali hiyo Meneja wa Shirika hilo Mkoani hapa ambaye pia ni Menejea wa shirika hilo Mkoani Shinyanga Gamba Maugira alikiri kuwepo kwa tatizo la kukatika umeme mara kwa mara na kudai sababu kubwa ni njia hiyo ya umeme kuwa ya siku nyingi na nguzo zake nyingine zimeoza na vikombe si salama.
Alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikichangia umeme kukatika mara kwa mara hasa nyakati hizi za mvua zenye kuambatana na upepo mkali na kujikuta nguzo zikianguka na vikombe kupasuka na hali hiyo inapotokea mafundi wa TANESCO huwa na wakati mgumu kurejesha umeme hasa nyakati za usiku.
0 Response to "WANANCHI MKOANI SIMIYU WALILALAMIKIA SHIRIKA LA UMEME TANESCO"
Post a Comment