Habari za hivi Punde

MADIWANI BARIADI WAKATAA KUPITISHA TAARIFA YA MAAFA KWA KUDAI NI MWAKA JANA







Baraza la madiwani la halmashauri ya mji wa Bariadi  mkoani Simiyu  limeikata taarifa ya maafa katika vijiji mbalimbali vilivyotokea na kudai kuwa ni ya mwaka jana huku afisa kilimo Issa Mtweve akishindwa   kuorodhesha vijiji vilivyoadhirika na janga  la njaa wilayani humo.

Wakiongea ndani ya kikao cha baraza hilo madiwani hao walisema kuwa vijiji vilivyokuwa vimeorodheshwa katika taarifa hiyo havikuwa sahihi, kutokana na kuwa vichache kulinganisha na hali halisi ya tatizo hilo lilopo katika kata zao.




Walibainisha kuwa tatizo la njaa katika kata zao ni kubwa sana kwa kila kijiji kuwa na njaa, ambapo walieleza kuwa taarifa hiyo ilidhorotesha baadhi ya vijiji na vingine kuachwa ambavyo ndivyo vilikuwa vimeadhirika zaidi kuliko vilivyoko kwenye taarifa hiyo.

Mmoja wa madiwani  kutoka kata ya Nyakabindi   Benjamini Matondi alisema kuwa  kuorodheshwa  kwa vijiji vichache katika kila kata kuwa ndivyo vilivyoadhirika tu, siyo kweli kwani kila kijiji ndani ya kata zao kimeadhirika, hivyo kumtaka Afisa huyo kufanya tadhimini upya kwa kuweka vijiji vyote katika kila kata vilivyoadhirika na njaa.
“Katika kata yangu nina vijiji zaidi 6 lakini hapa ninaona kuna vijiji 2 tu, na ndivyo vitakavyoletewa msaada wa chakula, wakati mimi ninavyojua vijiji vyote katika kata yangu vyote vimeadhirika na njaa na wala siyo hivi vilivyoko katika tarifa hii.”alisema diwani huyo.

Madiwani hao walikataa kupitisha taarifa hiyo na kumtaka Afisa kilimo huyo kufanya utafiti upya na kuhakikisha vijiji vyote ndani ya kila kata vilivyoadhirika na njaa vinaorozeshwa, ambapo waliongeza kuwa katika kufanya kazi hiyo upya ashirikiane na madiwani hao ili kubaini vijiji vilivyo na hali mbaya.


Mbali na hilo  taarifa hiyo ilionekana ni ya mwaka  2013  huku wakiikata kwa madai  siyo  sahihi  ambapo ofisa huyo alikiri kuwa taarifa hiyo ilikuwa ya mwaka huo huku akiwahakikishia madiwani hao kuandaa taarifa upya ambayo itakuwa sahihi.

0 Response to "MADIWANI BARIADI WAKATAA KUPITISHA TAARIFA YA MAAFA KWA KUDAI NI MWAKA JANA"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.