Habari za hivi Punde

ZOEZI LA UNYWAJI UJI KWA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI IHUGI HUENDA LIKASITISHWA KUTOKANA NA WAZAZI KUKOSA FEDHA ZA MICHANGO

ZOEZI  la  kunywa uji kwa wanafunzi wa  shule  ya msingi Ihugi kata ya Lyamidati   katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga huenda likasitishwa kutokana na shule hiyo kukosa chakula na wazazi kuwa na hali ngumu ya kifedha katika kusaidia upatikanaji  wa unga.

 Akiongea na mwandishi wa habari aliyetembelea shuleni hapo , mwalimu mkuu wa shule hiyo  Ayoub Mesoyo   alieleza  kuwa  shule imefunguliwa lakini zoezi la kupata uji shuleni hapo litasitishwa kutokana na ugumu wa kupata msaada wa mahindi na kifedha   kutoka kwa wazazi.

Mesoya akieleza kusitishwa huko alisema kuwa  ni kutokana na hali ngumu ya wazazi kifedha na mazao ambapo walikuwa wakichangia  mahindi kwaajili ya kupata unga sasa ni msimu wa kilimo  inaonekana kuwa vigumu kuchanga mpaka pale watakapo vuna  mazao.

Alisema shule hiyo  inaidadi ya wanafunzi zaidi ya 500 walikuwa wakipata huduma ya uji majira saa nne  asubuhi na kuendelea na masomo ila chakula cha mchana hawakuweza kufanikisha kuwapatia shuleni hapo.

“Unywaji uji utasitishwa  kwa wanafunzi   ikiwa  wamefungua watapata huduma hiyo kwa wiki moja zoezi la kuwashirikisha wazazi  lilikuwepo ila tatizo ni ugumu wa  fedha na mazao kwa kipindi hiki cha masika  zoezi litaendelea mpaka pale  watakapo vuna mazao  wazazi”alisema.

Hata hivyo diwani wa kata hiyo Leo Mayiku alisema kuwa  wanafunzi walikuwa wakipata uji kutokana na wazazi  kuchangia kiasi kidogo cha fedha na mahindi  kwa lengo la kupata uji  ambapo makubaliano hayo yalipatikana  katika mkutano wa hadhara.

Hata hiyo Mkurugenzi wa halmashauri hiyo  Mohamed Kiyungi alisema kuwa  kati ya shule 128 za msingi  shule 57 ndizo zinazopata chakula  cha machana na uji ikiwa pia  shule zote zilielezwa kutekeleza kilimo cha zao la mtama ili kuweza kujiendesha zenyewe bila kupata michango kutoka kwa wazazi.

Aidha  baadhi ya wazazi  Soja Mande na Kafulia James walisema kuwa   hali ya kifedha ikiwemo chakula katika familia imekuwa ni ngumu  na kupelekea hata baadhi ya kaya kula mlo mmoja kwa siku  na kushindwa kutoa michango mbalimbli katika shule hiyo  inayowakabili.
 
KARENY. Powered by Blogger.