Mkuu wa mkoa
wa shinyanga Ally Nassoro Rufunga juzi amezindua rasmi bodi ya hospitali ya
rufaa ya mkoa huku akiwataka wajumbe wa bodi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi ili
kuboresha mfumo wa uendeshaji wa hospitali ya mkoa wa shinyanga.
Bodi hiyo itakuwa na wajumbe 17 pamoja na mambo mengine inajukumu la kushirikiana na
wadau wote wa afya mkoani Shinyanga lengo likiwa ni kuboresha upatikanaji wa huduma hiyo.
Katika
uzinduzi wa bodi hiyo, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa, Rufunga ametoa rai kwa bodi hiyo kufanya vikao kwa mujibu wa
sheria pamoja na kusimamia vyanzo vya mapato ya fedha na matumizi ili kuongeza
kiwango cha huduma ya afya katika mkoa wa shinyanga.
Awali akiongea
katika uzinduzi huo mganga mkuu wa mkoa wa shinyanga Dkt Ramadhani Kabala amesema bodi hiyo
inatokana na mabadiliko endelevu katika sekta ya afya chini ya mkakati wa pili ambao
unalengo la kuimarisha uwezo wa hospitali za mkoa na kanda ili ziweze kutoa
huduma bora za rufaa.
0 Response to "MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AZINDUA BODI YA RUFAA YA MKOA"
Post a Comment