Habari za hivi Punde

MWENDESHA DALADALA YA BAISKELI ATUHUMIWA KWA UBAKAJI WA MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI NA KUMTOBOA MACHO

KIJANA   Omary  Simon (30) anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Shinyanga  kwa tuhuma ya kumbaka   mwanafunzi wa darasa la pili (9)  anayesoma katika  shule ya Msingi Kitangili Manispaa ya Shinyanga kisha kumtoboa macho  kwa kutumia kitu chenye ncha kali na kumuacha porini akisota kwa muda wa siku mbili.

Kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga  Evarist  Mangalla alisema tukio hilo lilitokea Aprili 20, mwaka huu majira ya saa 10;00 jioni katika kitongoji cha  Bugweto  nje kidogo ya mji  baada ya siku hizo aliokotwa na wanawake wawili.

Kamanda Mangalla alisema siku ya tukio mwanafunzi huyo ambaye nanaishi na Bibi yake Kata ya Ibinzamata alipewa shilingi 500/= na bibi yake kwa ajili ya kupanda Daladala  ya baiskeli kwenda kwa mama yake mkubwa anayeishi kata ya Ngokolo.

Mangalla  alisema alipofika katika kituo cha daladala  alikutana na mtuhumiwa  Simon  mwendesha  dalada ya baiskeli  ambaye alimpeleka katika Pori dogo la lililoko katika Kitongoji cha Bugweto na kumbaka na kisha kumchoma choma Macho kwa kitu chenye ncha kali na kumtelekeza katika eneo hilo bila ya msaada.

"Tangu Mwanafunzi  huyo atoweke kwao Aprili 20, alikuja kuokotwa Aprili 22, mwaka huu majira ya saa  4;00 asubuhi na wanawake wawili na kumpeleka katika kituo cha Polisi ambao walimpeleka hospitali  ya mkoa  hadi sasa anaendelea kupata matibabu “alisema  Mangalla.

Kamanda Mangalla alisema mtuhumiwa tayari amekwisha  kamatwa  na jeshi la polisi hivyo  atafikishwa Mahakamani  wakati wowote na iwapo atapatikana na hatia  ili kuweza kujibu shitaka hilo.

Akizungumza na Waandisi wa habari     bibi wa Mwanafunzi  huyo alisema amefungua  kesi katika Kituo cha kati cha Polisi  Jalada lenye kumbukumbu namba  SHY/RB/2098/2014 mara baada ya kuhisi mwijukuu wake amefanyiwa kitendo hicho kutokana na hali aliyonayo.

KARENY. Powered by Blogger.