WAZAZI na walezi wilayani Maswa mkoani Simiyu wamehimizwa kuona umuhimu wa chanjo kwa kuwapeleka watoto kupata chanzo mbalimbali za kuzuia maradhi ya kuhara na Nimonia zinazostahili kupatiwa kwa watoto walio chini ya mwaka mmoja ikiwa zaidi ya watoto 13,000 hawakupatiwa chanjo.
Changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa zoezi hilo ambazo ni pamoja na uelewa mdogo wa jamii kuhusu umuhimu na ukamilishaji wa chanjo zote,watotohao hawakupata au kukamilisha chanjo sabau ikielezwa ni ukosefu wa usafiri kwa ajili za kliniki za mkoba za chanjo kwa baadhi ya vituo vya
kutolewa huduma za afya.
Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dkt Jonathan Budenu alibainisha hayo katika uzinduzi wa wiki ya chanjo uliofanyika katika zahanati ya kijiji cha Malita kata ya Zanzui na kuhudhuria na baadhi ya wananchi hasa akina mama wachache waliojitokeza
.
“kiwango cha ufanisi kwa chanjo ya Pentavalent 3 inayozuia magonjwa matano ambayo Kifaduro,Dondakoo,Pepopunda,Homa ya Ini na Homa yaUti wa mgongo kimeongezeka kutoka asilimia 82 mwaka 2012 hadi asilimia 93 mwaka 2013”alisema dtk Budenu.
Alisema kwa wilaya hii kiwango cha ufanisi kwa chanjo ya
Pentavalent 3 kimeongezeka ikiwa mwaka 2012 hadi 2013 watoto zaidi ya 18,000 walichanjwa kati ya watoto 19,807 .
Naye mkuu wa wilaya hiyo Luteni Mstaafu Abdalah Kihato Alisema watoto ni binadamu dhaifu wanahitaji uangalizi wa karibu hawana wanachokijua isipokuwa kupata maziwa ya mama ikiwa chanjo zilizozinduliwa za kuhara(Rotavirus)na Nimonia(PCV 13) kwa watoto wa chini ya mwaka mmoja ni lazima kuzipata.
“Chanjo iliyokamilika ndiyo msingi wa kuwa na afya njema kwa mtoto na kuzuia maradhi mbalimbali yanayosumbua watoto hivyo itakuwa vigumu kwa mtoto kupata maradhi kwa sababu mwili utakuwa na kinga ya maradhi kwa miaka mingi”alisema Kihato.
Hata hivyo aliwataka wazazi kuwapeleka watoto wao kwenye vituo ili
kupatiwa chanjo hizo iwapo watatozwa fedha na muuguzi
yeyote wakati wa chanjo hizo ni kinyume cha utaratibu kwani hupatikana bure bila gharama yoyote.
0 Response to "WAZAZI WAHIMIZWA KUONA UMUHIMU WA CHANJO KWA WATOTO"
Post a Comment