BAADHI ya wazazi na walezi manispaa ya Shinyanga asilimia kubwa wamekuwa hawapendi kuchangia miradi ya maendeleo mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu hali ambayo imeonyesha katika shule ya sekondari Mazinge kushindwa kuchangia huduma ya wanafunzi kupata uji na chakula cha mchana.
Ikiwa kila mwanafunzi inatakiwa achangie kiasi cha shilingi 3000, hivyo Idadi ya wanafunzi waliotoa michango yao ni 6 pekee kwa shule nzima kati ya wanafunzi 664 kwa lengo la kupata uji wawapo shuleni hapo, imeelezwa wazazi ndio chanzo cha kudhorotesha kutokupata huduma hiyo ikiwa katika sherehe za harusi wanakuwa mstari wa kwanza kuchangia.
Diwani wa kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga David Nkulila,ambaye pia ni naibu meya wa manispaa hiyo aliyasema hayo wakati wa kikao cha kamati ya maendeleo ya kata hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya afisa mtendaji wa kata hiyo.
Nkulila alisema hayo baada ya kupewa taarifa na mkuu wa shule ya sekondari Mazinge iliyopo katika kata hiyo,kuhusu mchango kwa ajili ya wanafunz 664,ambapo kati ya hao 6 pekee wamechanga huduma ya uji tangu mwaka jana.
Nkulila alisema ni vyema sasa wananchi wakabadilika na kuona umuhimu wa kujali watoto kwamba tatizo siyo wananchi kukosa elimu bali kinachotakiwa ni wananchi kupewa hamasa na viongozi kuwa mstari wa mbele kuchangia.
“Wananchi wanahitaji hamasa siyo elimu,na katika hili sisi viongozi tunapaswa kuwa wa kwanza kuchangia hata kama hatuna watoto katika shule,mimi nilichangia magunia ya mahindi katika shule za kata hii,na nimetoa gunia la mchele katika shule ya sekondari Mazinge”,aliongeza Nkulila.
Naye mkuu wa shule ya sekondari Mazinge Henry Ntuah alisema sababu zinazopelekea wananchi kuwa nyuma kuchangia elimu mfano huduma ya chakula kwa wanafunzi ni wazazi na walezi kutohudhuria vikao vya shule pindi wanapohitajika.
Ntuah alisema wazazi wanaohudhuria vikao vya shule ni wachache matokeo yake utekelezaji wa mpango wa chakula kwa wanafunzi ikiwa ni agizo la mkuu mkoa wa Shinyanga kwa kila shule kupata huduma ya chakula na uji unakwama.
Nao wajumbe wa kamati hiyo mbali na kumpongeza diwani wa kata hiyo kuwa mstari wa mbele kuchangia sekta ya elimu katika kata yake ,ambapo mratbu elimu kata Seleman Bulugu alisema kuwa diwani aliweza kutoa michango ya magunia kumi na moja kwaajili ya shule tatu za msingi zilizopo kwenye kata huku wakitaka viongozi wengine kuiga mfano wake.
0 Response to "WAZAZI NA WALEZI WANASHINDWA KUCHANGIA MIRADI YA MAENDELEO."
Post a Comment