HALMASHAURI ya wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga imebaini kaya 5881 kutokuwa na vyoo ikiwa kaya 3335 zimejenga vyoo vya muda hali ambayo inaonyesha kuwa hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko hasa ya kuhara na kipindupindu.
Kaya hizo zilibainika wakati wa kampeni inayoendelea ya usafi wa mazingira na kuihamasisha jamii kuwa na vyoo bora katika kata zote za wilaya hiyo kwa kutumia sheria ndogo za halmashauri, huku mila na desturi zikitajwa kuwa ni chanzo cha kuwepo tatizo hilo na kuona ni muhimu kwa kujisaidia vichakani.
Akizungumza na waandishi wa habari afisa mazingira wa wilaya ya Kishapu Mohamed Mlewa, alisema wilaya inakaya 42,000 kati ya hizo zenye vyoo bora ni 12,680 vya kawaida 20,114 na ambavyo vimejengwa kwa matumizi ya muda ni 3335 huku kaya 5881 vikiwa havina vyoo .
“Ni muhimu kila kaya iwe na choo tena tunasisitiza kiwe bora na ndiyo maana tunaendelea kutoa elimu kwa jamii, iweze kubadilika iache mila na desturi zilizopitwa na wakati kama sasa hivi tumebaini kuwepo kaya 5881 zisizokuwa na vyoo hata vya muda hawana”alisema Mlewa.
Alisema walitembelea kata za Masanga ,Shagihilu,Mwamashele na Ukenyenge ambapo walizungumza na wananchi na kutoa elimu sanjari na kukagua kaya kama zinavyoo nakukuta baadhi hazina ambazo walizitaka kuhakikisha wanachimba haraka il kuzuia kuibuka magonjwa ya mlipuko.
Ameitaka jamii kubadilika kwa kuhakikisha mazingira wanayoishi yanakuwa safi ,hatua itakayosaidia kujiepusha kukumbwa na kipindupindu hasa kipindi hiki cha mvua za masika zinazoendelea kunyesha, ambapo hutokea mlipuko wa magonjwa mbalimbali mazingira yakiwa machafu.
Wakati huo huo ilibainika pia kukosekana kwa miundombinu bora ya maji na vyoo pamoja na mazingira machafu umesababisha nyumba za kulala wageni tatu na hoteli mbili kufungwa, katika halmashauri hiyo.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya idara ya usafi wa mazingira wilayani humo kufanya ukaguzi na kubaini kuwepo changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa maji,kalo la maji machafu na miundombinu ya ndani kutoridhisha yakiwemo mashuka hivyo kuhatarisha afya za wateja.
.“Hili zoezi lilifanyika march 27 mwaka huu katika mji wa mhunze ambapo tulifunga hotel mbili na kisha mji mdogo wa Maganzo hoteli moja na nyumba za kulala wageni mbili,tunaendelea na zoezi hili kwa wilaya nzima ili kuhakikisha mazingira yote yanakuwa safi ”alisema Mlewa.
Afisa mazingira alisema zoezi hilo limeanza kwa kupitia hoteli na baa na kwamba hatua itakayofuata ni kukagua migahawa,ambapo aliwataka wananchi kuhakikisha wanaweka mazingira katika hali ya usafi ili kuzuia mlipuko wa magonjwa ambao unaweza kutokea kwa kusababishwa na uchafu.
0 Response to "HALMASHAURI WILAYA YA KISHAPU IMEBAINI KAYA 5881 KUKOSA VYOO"
Post a Comment