Habari za hivi Punde

CHANGAMOTO KUBWA INAYOWAKUMBA WATOTO KWEYE KITUO MAAMULU CHA WALEMAVU BUHANGIJA NI UHABA WA VITANDA




CHANGAMOTO kubwa inayowakabili watoto  kwenye kituo  maalumu cha kulea watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali cha Buhangija manispaa ya Shinyanga, ni upungufu  wa vitanda hali inayowalazimu kulala watatu watatu  kutokana na kutokidhi mahitaji ambapo vilivyopo ni 156 huku watoto wakiwa 258.

Hayo yalielezwa  na mwalimu mkuu wa  shule ya Buhangija ambaye anasimamia kituo hicho,wakati akipokea msaada wa chakula,sukari na mafuta kutoka kwa mbunge wa viti maalumu(CCM) mkoa wa Shinyanga Azza Hamad,aliyetembelea kituo hicho.

Ambapo mbunge huyo alijionea  kero mbalimbali zinazowakabili watoto hao ukiwemo upungufu wa mabweni pia yaliyopo ni matatu yenye uwezo wa kuchukua watoto 100 pekee.

“Wakati wa kulala kwenye mabweni utawaonea huruma watoto hawa,kunakuwa na msongamano mkubwa inatubidi wale wadogo wadogo walale watatu watatu kitanda kimoja kama unavyoviona vitanda vyenyewe ni vidogo vinafaa mtu mmoja ,tunaomba wahisani mbalimbali watusaidie kujenga bweni na kuongeza vitanda ”alisema mwalimu Ajali.

Mwalimu ajali alisema kuwa,msongamano wa watoto umekuwa mkubwa  kwani mwaka 2008 wimbi la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi(Albino) liliibuka ndipo serikali iliamua kuchukua jukumu la kulea watoto hao wakiwemo albino,wasioona na viziwi  lengo kuwaweka kwenye ulinzi.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu Azza Hamad,alisema ni jukumu la kila mmoja kuwasaidia watoto hao na kuzitaka halmashauri zote ambazo watoto wake wanalelewa kwenye kituo hicho, kutoa michango yao badala ya kuiachia manispaa na wilaya pekee kubeba jukumu hilo wakati mikoa jirani ya Simiyu,Tabora  na Geita ikishindwa kutoa michango ya kusaidia kituo hicho.

Azza alisema watoto hao wana haki ya kupatiwa huduma muhimu kama watoto wengine ikiwemo elimu,afya bora,malezi na kuishi badala ya kuwatelekeza na kuwaacha,ambapo aliahidi kuendelea kutoa mchango wake ikiwa ni pamoja na kuwagharamia mahitaji muhimu watoto wote wakike watakaofaulu kwenda sekondari.

Diwani  wa kata ya Buhangija Mathew Matemu,alisema huyo ni mbunge wa kwanza kutembelea kituo hicho baada ya kuguswa na changamoto zinazowakabili watoto hao,nakuwataka viongozi wengine kuiga mfano huo kwa kuona umuhimu wa kusaidia kundi hilo maalumu linalohitaji michango ya wahisani,mashirika na watu binafsi.

0 Response to "CHANGAMOTO KUBWA INAYOWAKUMBA WATOTO KWEYE KITUO MAAMULU CHA WALEMAVU BUHANGIJA NI UHABA WA VITANDA"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.