UMOJA wa vijana wa
chama cha Mapinduzi kanda ya ziwa (UVCCM)
umewataka watanzania kutokubali muundo wa serikali tatu na kuwaeleza kuwa
iwapo zitakuwepo hizo serikali upatikanaji wa fedha zinazotokana na
ulipaji kodi hazitatosheleza ikiwa jamii bado zinahitaji
huduma bora kwenye afya,elimu na mambo
mengine .
Hayo wameyasema
kwenye matembezi ya mbio za pikipiki ya muungano taifa
yaliyoandaliwa na umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM)
taifa ambapo matembezi hayo yalikuwa yamebeba ujumbe wa
dumisha muungano vijana kwa fursa zilizopo kwa
maendeleo yetu, kwa mkoa wa shinyanga yalipokelewa kutoka mkoani
Simiyu katika kijiji cha Wigelekelo wilayani Maswa.
Kiongozi wa matembezi ya
mbio hizo kanda ya ziwa Zuberi Bundala alisema kuwa wameamua
kuzunguka wilaya zote za kanda kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi
ikiwa baadhi ya vyama wanadai kuwepo kwa serikali tatu jambo ambalo
litafanya jamii kukosa mambo ya msingi kwa kupitia kodi wanazolipa.
Akitoa ujumbe huo
katika mikutano ya hadhara kwa nyakati tofauti kwa wananchi
wa wilaya ya Kishapu na Manispaa ya Shinyanga Bundala
alisema kuwa serikali mbili ndizo zinatoa fursa ya mwananchi kuona kodi
yake inatumika vipi kuliko hiyo serikali tatu ambayo inapiganiwa na baadhi
ya vyama ,hivyo wapiganie wao hizo serikali na kutoa hoja za msingi
kwa wananchi .
Alisema
kwa mujibu wa taarifa ya maoni ya wananchi kupitia rasmu ya katiba
iliyowasilishwa na aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya
katiba Joseph Warioba kwenye bunge maalumu la katiba mjini Dodoma
alisema kuwa asilimia 61 imependekeza serikali
tatu hivyo vijana watahakikisha wanapigana kutetea maslahi ya
wananchi kwa kutaka serikali mbili.
“Sisi kama vijana wa
chama cha Mapinduzi tunataka serikali mbili ambazo wananchi wanalipa kodi na
kuona matokeo ya kodi zao sasa ije hiyo serikali tatu kodi itaonekanaje?,
kama vyama vya upinzani wanataka serikali tatu waipiganie na kutoa hoja
za msingi , hivyo wajumbe ambao ni wabunge wa bunge la katiba nao
wanaonekana kushindwa basi warudi nyumbani na kurudisha pesa walizozitumia
mpaka sasa,vijana tumeahidi kupigana na kutaka maslahi ya wananchi
yasipotee.”alisema.
Naye mwenyekiti wa umoja
wa vijana CCM mkoani wa Shinyanga Mapinduzi Henry
alisema kuwa muundo wa serikali mbili ndio unaofaa hivyo vijana
wasikimbilie serikali tatu ambazo kwa kuangalia malengo yake
baadaye ni kuwakandamiza wenye kipato cha chini ikiwa wanatumia kodi zao kupata
maendeleo hiyo nyingine ya tatu ni mzigo kwa wananchi.
Hata hivyo mbunge
Selemani Nchambi kutoka jimbo la Kishapu na mbunge
Steven Masele kutoka jimbo la Shinyanga mjini walisimama kwenye mikutano
hiyo ya hadhara huku kila mmoja katika jimbo lake akiwaeleza wananchi kukataa
kwa serikali tatu na kueleza faidi zinazopatikana
kwenye muungano wa sasa kuwa anayetoka Zanzibar anamiliki ardhi ya
Tanzania bara bila wasiwasi huku kodi zikimnufaisha
mlipa kodi wa Tanzania bara.
Katibu wa chama
cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Adamu Ngalawa alisema
kuwa suala la serikali tatu litaonyesha kuwatenga baadhi ya raia
ikiwa kunamzaliwa kutoka Tanzania bara na Zanzibar na mwingine hayuko
pande zote sula la kujiuliza watapewa uraia wa upande upi ?.
Ambapo mwenyekiti wa
chama hicho mkoa Khamis Mgeja alisema kuwa baadhi ya watu
wanaubeza muungano huku wengine wakidai hati ya muungano,kazi kubwa
iliyopo sasa ni kutetea Tanzania na msimamo uwe wa serikali mbili ikiwa wakati
wa uchaguzi mwaka 2010 sera zilizowasilishwa za kila chama , lakini sera
ya CCM ilionyesha ni jinsi gani bado inahitaji serikali mbili na muungano
bado haujapoteza uhalisia wake.
Hata hivyo matembezi
hayo ya kuuenzi muungano wa miaka 50 wa Tanzania bara na
Zanzibar ulinzinduliwa rasmi tarehe 22 march mwaka huu
na rais wa Zanzibar Dtk Mohamed Shein huku kanda ya ziwa
yalianza rasmi tarehe 11 mwezi huu mkoani Mara.
0 Response to "UMOJA WA VIJANA CCM (UVCCM) KANDA YA ZIWA WATAKA MUUNDO WA SERIKALI MBILI"
Post a Comment