Habari za hivi Punde

MZAZI ATINGA SHULENI NA BAKORA KISA ATAKA BINTI YAKE AKAELEE MTOTO NYUMBANI.
MZAZI wa Mgreth  Tilu anayesoma  shule ya msingi  Bugimbagu darasa la saba  iliyopo kata ya Mwawaza  manispaa ya Shinyanga  alitolewa  darasa na baba yake mzazi  huku akiwa ameshika fimbo  mkononi  kwa kumtaka arudi nyumbani  kwa lengo la kwenda kumlea  mdogo wake.

Mzazi huyo aliyefahamika kwa jina la Tilu Bushi alifanya kitendo hicho  katika shule hiyo wakati  muda  wa kufanya  mtihani  wa mocko  ukiendeleo ndipo aliamua  uamuzi wa kumfuata shule  na kusababisha  mwanafunzi  huyo  kushindwa  kufanya mtihani wake.


Ambapo tukio hilo  lilitokea juzi  majira ya saa tatu asubuhi shuleni hapo huku baadhi ya walimu wakishirikiana kutoa  taarifa kwa jeshi la polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe zaidi,kutokana na kitendo cha kumnyima haki ya  msingi mtoto.

Hata hivyo baada  ya taarifa kutolewa  mzazi huyo alikimbi na kutokomea kusikojulikana huku jeshi la polisi likiendelea kumsaka kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Evarist Mangalla alisema tukio hilo lilitokea wakati  mwanafunzi huyo akiwa anafanya mtihani wa mocko wa darasa la saba, ikiwa  mzazi wake alifika  na kuingia darasani kisha kumtaka  binti yake arudi nyumbani kulea mtoto.

Kamanda Mangalla alisema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mzazi huyo  kwa lengo la  kufikishwa kwenye vyombo vya sheria  kutokana na tuhuma inayomkabili.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga  Annarose  Nyamubi  alisema  kwa  kitendo  hicho alichokifanya mzazi huyo  sio kizuri  hasa  kufanyiwa mtoto wa kike  ambapo jamii inaelimishwa kila siku kuwapatia elimu watoto ili kuweza kupata taifa lenye wasomi na kuweza kujitegemea.

“Mzazi huyo anatakiwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili liwe fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo pamoja na kukumbushwa  majukumu  yao  katika kuhakikisha mtoto anapata elimu bila kubaguliwa  na anayeshindwa kumsomesha mtoto  bila sababu za msingi  atachukuliwa hatua  za kisheria.”alisema


 


KARENY. Powered by Blogger.