WAWEKEZAJI manispaa ya Shinyanga wamelalamikiwa
kutotekeleza matakwa waliyokubaliana mara baada ya kuwa wameomba
kuwekeza maeneo mbalimbali na kuchukua ardhi kubwa jambo ambalo limefanya
kuzua migogoro mikubwa kwenye maeneo ya wakazi hao.
Kitu kilichobainika mara baada ya kukaa kamati ya
miundombinu ya madiwani,ilijionea mwekezaji katika eneo la N’helegani
alichukua ekari zaidi ya 100 huku akiahidi kujenga madarasa
kwaajili ya kuanzisha shule ya wakulima , kuajiri wafanyakazi wazawa huku
wawekezaji wengine wakiahidi pia kuweka kiwanda cha kusindika
nyama mambo ambayo yamekwenda kinyume.
Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa kamati ya miundombinu
ambaye pia ni diwani wa kata ya Chamaguha Morice Mghin
kwenye baraza la madiwani lililofanyika katika ukumbi
wa mkoa huku akieleza kuwa kutokana na makubaliano hakuna madarasa
yaliyojenga wala shule, hakuna ajira iliyotolewa matokeao yake
wananunua marobota na kutenge nyuzi kwa kusafirisha nje ya nchi.
“Jambo lingine wawekezaji kampuni ya
wachina eneo la ibadakuli tulikubaliana kiwanda cha kusindika
nyama wanachokifanya wanasindika ngozi pekee tena
wameajiri vijana wanaowatumia bila vitendea kazi mikono yao imeanza
kuchumbuka hivyo wanaonekana kutotii sheria ya Osha,huku
mwekezaji kampuni ya jambo akilalamikiwa kuchukua eneo zaidi
tofauti na alivyopimiwa hali ambayo imezua migogoro kwa wananchi wa eneo
hilo na kiasi cha zaidi ya shilingi millioni 400 bado
hakijalipwa.”alisema Mghini.
Hivyo alitoa ushauri kuwa suala la wawekezaji
limeonyesha kuwa na ubabaishaji kila wanapofuatwa hukumbilia kwa
mkuu wa mkoa utaratibu uwepo wa wawekezaji kupitia kwa
wakurugenzi wanaotoa ardhi na uwe wa hisa na sio
uanzie mkoani kama ulivyo sasa ambapo imeonekana wananchi
kuwakosesha haki zao za msingi.
Diwani wa kata ya Ibadakuli Leonard
Richard alisema kuwa kumekuwepo mgogoro wa ardhi eneo
hilo kampuni ya jambo kuchukua eneo zaidi huku Siri
Yasin diwani viti maalumu akieleza kuwa baadhi ya
watumishi wamekuwa wakiegemea upande wa wawekezaji bila kushirikisha
wananchi jambo ambalo linaonyesha kujidhalilisha ikiwa wanatakiwa
kuanzia uongozi wa vitongoji,vijiji na kata ambapo kunapatikana ukweli
sio kwenda kwa mwekezaji.
Naye naibu mstahiki meya wa manispaa David
Nkulila alisema kuwa hakuna sheria inayoua sheria wawekezaji
wamekuwa wakienda kinyume na kuleta ubabaishaji ikiwa wameonekana
dhahiri pindi wanapofuatwa na maafisa mbalimbali hujifanya
kutofahamu lugha hasa hawa wachina na mwisho wa siku humfuata mkuu
wa mkoa na kutoa malalamiko yao.
Kaimu mkurugenzi ambaye pia ni ofisa ardhi wa
manispaa Dismas Minja alisema kuwa yanayosemwa ni kweli
ila kinachotakiwa ni kuanza ufuatiliaji wa karibu ili
wananchi wanufaike na ardhi yao, hivyo inatakiwa kuwa macho na
wawekezaji wa namna hii haiwezekani wanachukua ekari 150 na hakuna kitu
chochote kinacho fanyika kwa wananchi.
Katibu tawala wilaya. ya Shinyanga Boniface Nchambi alisema kuwa
suala la mgogoro wa ardhi limekuwa ni changamoto kubwa kwenye
maeneo yaliyochukuliwa na wawekezaji hivyo uamuzi uliopo
waorosdheshwe watu wote waliochukuliwa maeneo yao ili kuweza
kubaini tatizo liko wapi.
0 Response to "WAEKEZAJI MANISPAA YA SHINYANGA WALALAMIKIWA."
Post a Comment