MWENYEKITI wa chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani
Simiyu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Busega dkt Titus Kamani
ameendelea kusisitiza muungano wa serikali mbili kwa sababu waasisi wa
wazamani wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Abed Karume walikaa na
kujadili mafanikio ya muungano wa Tanzania na kusisitiza uwepo wa serikali
mbili.
Mbunge huyo ambaye ni waziri wa maendeleo ya uvuvi na mifugo
alisema ni busara za waasisi hao za kusistiza muungano na kuenzi
zilizopelekea kuundwa kwa muundo wa serikali mbili zimesababisha hali ya muungano
mpaka sasa kuwa imara na kuleta amani baina ya watanzania, na kutaka muundo huo
ni vyema ukaendelea ili kulinda muungano.
Kamani alisema hayo juzi katika mapokezi ya pikipiki
ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi ccm kutoka Mkoani Mara na Mkoa wa
Simiyu yenye lengo la kuwaunganisha vijana kuwa na ushirikiano na kuleta amani
na utulivu nchini.
Alisema wapo watu ambao kupitia katika siasa wanajaribu
kuharibu muungano wa Tanzania kwa sababu tu wao wanamasilahi yao binafsi na
vyama vyao wala sio kwa ajili ya kuleta maendeleo hapa nchini ili
wananchi waweze kujikwamua kimaendeleo.
Alisema kuwa bunge la katiba kwa sasa limejikita
katika kujadili mambo ya muungano lakini kwa vyama vyote vya upinzani
vinataka kuwepo na serikali tatu za Serikali ya Zanzibar,Tanganyika na ya
Muungano kwa kutokutambua waasisi wa muungano huo walijadili kwa kina kuhusu
muungano huo.
“Kwa sasa jicho la watanzania linatazama bunge
lakini unashangaza wabunge kutoka vyama vya upinzani wanapoingia bungeni
kuanza kupinga, huku katika kamati zao wao huwa wanakubaliana”alisema
Kamani.
Alisema suala la serikali tatu linahitaji gharama kubwa
katika kuendesha shughuli zake, sambamba na kuwepo kwa hali vurugu kama ilivyo
katika mataifa ya sudani, Tuisia pamoja na Somalia chanzo kikubwa kikiwa ni
mgawanyo wa mali.
Hivyo aliwataka wananchi kusoma kwanza
rasimu hiyo itakapofika kwa ajili ya kupigia kura pamoja na kuwa makini
kupiga kula wasije wakaamua kitu kikawa na madhara,wajumbe wapige kura
serikali mbili kutokana na kuizoea hivyo hakutajiki marekebisho yeyote
zaidi ya kuboresha muungano.
0 Response to "MWENYEKITI CCM MKOANI SIMIYU ASISITIZA WANANCHI MUUNGANO WA SERIKALI MBILI"
Post a Comment