Habari za hivi Punde

HALMASHAURI YA WILAYA YA BARIADI INAKABILIWA NA ZAIDI YA WANAFUNZI 450 HAWAJUI KUSOMA WALA KUANDIKA
HALMASHAURI  ya wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, inakabiliwa na idadi kubwa ya wanafunzi wa shule za msingi wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK), kutokana na uwajibikaji mdogo wa walimu na kutofundisha kwa vitendo, ikiwemo msongamano mkubwa wa wanafunzi madarasani.

Jumla ya wanafunzi 4999 ikiwa ni asilimia 8.5 ya wanafunzi wote katika wilaya , wasichana wakiwa 2660 asilimia 8.8, na wavuluna wakiwa jumla 2339, ikiwa ni asilimia 8.1, wote hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu, hali inayosababisha kiwango cha taaaluma kushuka wilayani hapa.

Hayo yalibainishwa na Afisa Elimu wa Halmshauri hiyo Doreen  Lutahamilwa, katika maazimisho ya wiki ya elimu yaliyofanyika juzi katika shule ya Msingi Mwamijondo iliyoko kata ya Sakwe.

Afisa elimu huyo alisema kuwa changamoto hiyo imekuwa kubwa kwa sasa katika wilaya hiyo, ambapo uongozi wa elimu ulibaini kuwa moja ya sababu kubwa inayosababisha kukua kwa hali hiyo ni uwajibikaji mdogo wa walimu katika kufundisha.

Alisema mbali na hilo uhaba wa madawati ambao upelekea wanafunzi wengi kukaa chini, pamoja na uchache wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia vimekuwa vikwazo katika kuhakikisha wananfunzi wanapata elimu bora ikiwa na kujua kusoma, kuhebu na kuandika.

Katika  kupambana na hali hiyo alisema  ofisi yake imeagiza walimu wakuu wote katika wilaya kuhakikish a wanawatambua wananfunzi wote wasiojua KKK, na kuwatenga ili wafundishwe kwa muda maalum, ikiwa pamoja na kuandaa utaratibu wa semina kwa ajili ya kuwawezesha walimu wanaofundisha darasa la awali na darasa la kwanza.

Kwa upande wake mwanyekiti wa halmshauri hiyo Bahati Mgamula ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maazimisho hayo alishtushwa na hali hiyo na kusema kuwa anapata mashaka na taaluma za walimu wanaoajiliwa katika halmshauri yake, ambapo aliutaka uongozi wa halmashauri kuanzisha oparesheni ya kuwawajibisha walimu watakaobainika kuwa chanzo  cha baadhi ya matatizo.
KARENY. Powered by Blogger.