CHANGAMOTO
inayowakumba mashirika ya umma nchini ni kuibiwa kwa miundombinu
mbalimbali ya vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi
wa miundombinu mbalimbali
ambapo shirika la umeme (TANESCO) mkoani
Shinyanga limeeleza kupata hasara kiasi cha shilingi millioni 9.5
kwa mwaka 2012 huku shirika la
mawasiliano mkoani Shinyanga (TTCL)
likipata hasara ya zaidi ya shilingi
millioni 108.
Ambapo Shirika la Reli
(TRL) kwa wizi wa Mataluma ya kwenye
barabara wameeleza kuwepo kwa biashara ya vyuma
chakavu,kutumia kwenye majembe
yanayokokotwa na ng’ombe pamoja na shirika la mawasiliano nchini TTCL wakieleza baadhi ya wakulima kuchimbua
nyaya zilizopo ardhini zinazohusika kupita kwa mkongo wa
mawasiliano wa Taifa.
Hayo waliyasema
kwenye mkutano wa viongozi wa
sungusungu uliofanyika kwenye uwanja wa
Kolandoto katika kata hiyo kwa
kukutanisha wilaya tatu za
Kishapu, Manispaa na Shinyanga
mkoani hapa huku ajenda kuu zikiwa mbili za ulinzi wa miundombinu na mahudhurio kwa wanafunzi mashuleni.
Ambapo ajenda ya ulinzi wa miundombinu viongozi wa
mashirika hayo walianza kutoa ufafanuzi
mbele ya jeshi la sungusungu namna gani wanavyopata hasara kutokana na
miundombinu kuibiwa au kuharibiwa na jamii wasiopenda maendeleo ikiwa
ofisa mahusiano wa shirika la umeme Tanesco
Michael Amon alisema
shirika hilo limepoteza kiasi cha shilingi Billioni 3.5 kutokana na wizi wa nyanya au vyuma katika transfoma
pekee.
“Unapohujumu
miundombinu ya Tanesco
ni kuipatia nchi hasara kubwa
ikiwa uchumi unashuka ,mawasiliano yatakosekana watoto watafeli shule kutokana na kutegemea masomo mengine nishati ya umeme hivyo viongozi wa
sungusungu mnatakiwa kuwa mabalozi kwa
wananchi kutoa elimu na kuwabaini
wanaofanya uhalibifu huo lengo ni kujinufaisha kwa matumizi yao binafsi
kisheria ni kosa”alisema Amoni.
Naye mhandisi wa
Tanesco Job Bidya alisema kuibiwa
kwa vipande vya vyuma 107 kwenye
laini inayopeleka umeme Mgodi wa
Bulyanhulu gharama yake ni shilingi millioni 9.5
ambayo serikali imeingia hasara hiyo
ikiwa mgodi huo ulikosa umeme kwa
siku 14 uliweza kupata hasara
kwenye uzalishaji kiasi cha
shilingi zaidi ya billioni 14.
Meneja wa shirika la mawasiliano TTCL mkoani Shinyanga Peter
Kuguru alisema kuwa miundombinu
ya shirika hilo imekuwa ikiharibiwa hasa na wakulima wanaolima kando ya
barabara palipochimbiwa nyaya zinazopita mkongo wa mawasiliano wa
Taifa na kufanya mawasiliano yakiwemo
ya mitando kwenye maofisi,mabenki
hospitalini kushindwa kufanya kazi sababu kuu ikiwa ni uhalibifu.
Kuguru alisema kuwa
hujuma inayofanywa na baadhi ya
watu kukata nyaya hizo bila kwenda
kuifanyia shughuli yoyote ikiwa cable moja gharama yake zaidi ya shilingi
millioni 10 kwa hasara inayopatikana,
ambapo mwezi Novemba mwaka jana hadi leo hii hasara iliyopatikana ni zaidi
ya shilingi millioni 108.
Naye mwakilishi wa shirika la reli kutoka mkoani Mwanza insp Suzan
Kidiku alisema kuwa miundombinu
ya reli ni
jukumu la kila mwananchi kuilinda kwa kuwa ndio njia ya kurahisisha
usafirishaji wa bidhaa na abiria ikiwa jamii
imekuwa haitoi ushirikiano wa kubaini
wanaofanya uhalibifu huo huku wengine wakitumia kama spea za kwenye majembe ya kukokotwa na ng’ombe na
kupeleka kuuza katika biashara ya vyuma chakavu.
Baadhi ya viongozi wa sungusungu akiwemo Jackob Charles katibu wa
sungusungu kutoka tawi la Mwalukwa wilaya ya Shinyanga na Selemani Kanoni kutoka tawi la
Ikonongo wilaya ya Kishapu walisema kuwa
wanashindwa kuwakamata kutokana na sungusungu kukosa nguvu ya kuwa na silaha ikiwa wanaohujumu uchumi
huja na silaha hivyo wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kukomesha wizi
huo.
0 Response to "MASHIRIKA YA UMMA YAPATA HASARA KUBWA KUTOKANA NA KUIBIWA KWA MIUNDOMBINU YAKE"
Post a Comment