Habari za hivi Punde

MWANAMKE ALIWA FISI SHAMBANI KWAKE AKICHUMA MBOGA
MKAZI  mmoja wa kijiji cha Giriku  kata ya Bunamhala  wilayani Bariadi mkoani Simiyu  aliyefahamika kwa jina la Nshoma  Mawe (29) amepoteza maisha  baada ya kuvamiwa na fisi kisha kun’gata wakati akiwa shambani nyumbani  kwake akichuma mboga.

Kwa mujibu wa  taarifa ya kamanda wa jeshi la polisi  mkoani humo  Charles Mkumbo  aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake amesema  kuwa tukio hilo  limetokea mnamo  majira ya saa 6:00 jioni.


Kamanda amesema  kuwa  mwananmke  Nshoma alivamiwa na mnyama huyo   akiwa shambani kwake akichuma mboga  shambani ghafla alitokea  na kuanza kumshambulia.

 Aidha  amesema wakati mwanamke huyo akiwa anachuma mboga shambani akiwa na ndugu zake, gafla alijitokeza fisi kisha kuanza kumshambulia na kumtenganisha kichwa pamoja na kiwili wili kisha kufariki papohapo.

 Hata hivyo amesema kuwa msako  unafanyika dhidi ya kumsaka   mnyama huyo   kwa kushirikina  wananchi na  jeshi la polisi.
KARENY. Powered by Blogger.