MTU mmoja
aliyejulikana kwa jina la Shija Mfuko (60) mkazi wa kijiji cha Zobogo kata ya
Itwangi tarafa ya Itwangi wilaya ya Shinyanga amekutwa amekufa kwa kujinyonga
kwa kutumia kamba ya katani katika shamba la mapera lililopo mpakani mwa kijiji
hicho na kijiji jirani cha Nhumbili kata ya Tinde wilayani humo.
Wananchi
walioshuhudia tukio hilo waliiambia sungwakareny.blogspot.com kuwa, walimkuta mzee huyo amejinyonga kwenye shamba
la mapera jana Jumatano majira ya saa 11 jioni huku wakidai kuwa huenda kifo
hicho kimetokana na kuchanganyikiwa kwa mzee huyo baada ya kuugua kwa muda
mrefu.
Mashuhuda hao waliongeza
kuwa siku hiyo ya Jumatano marehemu aliaga muda wa asubuhi kuwa anaenda kufanya
mazoezi kutokana na kwamba alikuwa amefanyiwa oparesheni ya tumbo lakini wakashangaa
kwanini hakurudi mapema ndipo wakaanza kumtafuta na kumkuta amejionyonga kwenye
shamba la mapera.
Akizungumza na
mwandishi wa habari mtoto wa marehemu
aitwaye Shija Mathias alisema ni kweli baba yake alikuwa amefanyiwa oparesheni
ya tumbo mwezi Juni mwaka huu,na tayari alikuwa amepona na kila siku amekuwa
akifanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya kuimarisha afya yake.
"kifo hiki
kinasikitisha sana na kimetushitua ,kwani mzee amekuwa akifanya mazoezi kama kawaida
leo kaondoka asubuhi hakurudi tena hajarudi muda mrefu ndiyo tukaanza kumtafuta
na polisi wameturuhusu kuuchukua mwili wa marehemu,na hapakuwa na mgogoro
wowote hapa nyumbani",alisema Mathias.
Kwa upande wake
afisa mtendaji wa kijiji cha Zobogo Elizabeth Gabriel alisema kifo cha mzee Jondo huenda kimetokana na
kuchanganyikiwa kwani alikuwa ameugua kwa muda mrefu na inasemekana kuwa kidonda
cha oparesheni kilikuwa kinatoa maji maji.
“Kutokana
na taarifa nilizozipata marehemu pia alitoroka siku moja kabla ya tukio
alitoroka lakini ndugu zake walifanikiwa
kumpata mzee huyo akiwa amejinyoga.
Mwisho.
0 Response to "ajinyonga"
Post a Comment