Habari za hivi Punde

ajinyongaMTU mmoja aliyejulikana kwa jina la Shija Mfuko (60) mkazi wa kijiji cha Zobogo kata ya Itwangi tarafa ya Itwangi wilaya ya Shinyanga amekutwa amekufa kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani katika shamba la mapera lililopo mpakani mwa kijiji hicho na kijiji jirani cha Nhumbili kata ya Tinde wilayani humo.

Wananchi walioshuhudia tukio hilo waliiambia sungwakareny.blogspot.com kuwa, walimkuta mzee huyo amejinyonga kwenye shamba la mapera jana Jumatano majira ya saa 11 jioni huku wakidai kuwa huenda kifo hicho kimetokana na kuchanganyikiwa kwa mzee huyo baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mashuhuda hao waliongeza kuwa siku hiyo ya Jumatano marehemu aliaga muda wa asubuhi kuwa anaenda kufanya mazoezi kutokana na kwamba alikuwa amefanyiwa oparesheni ya tumbo lakini wakashangaa kwanini hakurudi mapema ndipo wakaanza kumtafuta na kumkuta amejionyonga kwenye shamba la mapera.
Akizungumza na mwandishi wa habari  mtoto wa marehemu aitwaye Shija Mathias alisema ni kweli baba yake alikuwa amefanyiwa oparesheni ya tumbo mwezi Juni mwaka huu,na tayari alikuwa amepona na kila siku amekuwa akifanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya kuimarisha afya yake.
"kifo hiki kinasikitisha sana na kimetushitua ,kwani mzee amekuwa akifanya mazoezi kama kawaida leo kaondoka asubuhi hakurudi tena hajarudi muda mrefu ndiyo tukaanza kumtafuta na polisi wameturuhusu kuuchukua mwili wa marehemu,na hapakuwa na mgogoro wowote hapa nyumbani",alisema Mathias.
Kwa upande wake afisa mtendaji wa kijiji cha Zobogo Elizabeth Gabriel alisema  kifo cha mzee Jondo huenda kimetokana na kuchanganyikiwa kwani alikuwa ameugua kwa muda mrefu na inasemekana kuwa kidonda cha oparesheni kilikuwa kinatoa maji maji.
“Kutokana na taarifa nilizozipata marehemu pia alitoroka siku moja kabla ya tukio alitoroka lakini ndugu zake   walifanikiwa kumpata mzee huyo akiwa amejinyoga.
Mwisho.

KARENY. Powered by Blogger.