JAMII mkoani Shinyanga imetakiwa kujiombea na
kuliombea taifa katika mchakato huu wa kuunda katiba mpya kwenye
msimu huu wa kumalizika kwa mateso ya yesu kristo aliyejitoa na
kusulubiwa msalabani kwaajili ya dhambi za wanadamu huku akiwataka
kutenda yaliyo mema duniani.
Hayo yalisemwa jana na mchungaji
peter Msengi wa kanisa la Moravian lililopo
Ngokolo kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga katika ibada ya siku
ya ijumaa kuu mbele ya waumini wa kanisa hilo huku ikiwemo imani kutoka
kwenye kitabu cha maandiko kuwa binadamu hana kosa na kufikia
hatua ya kukiri mwenyewe.
Mchungaji Msengi alisema kuwa katika
ibada hiyo ujumbe uliotolewa, binadamu anaweza kubadilika hivyo
jamii imetakiwa kujiombea kutokana na changamoto wanazokabiliana nazo
ikiwemo kuliombea taifa na mchakato unaoendelea wa kuipata katiba
mpya.
“Ninanukuu maandiko yesu alisema imekwisha maana yake
alijitoa sababu ya dhambi zetu baada ya kupata adhabu zote
ikiwemo kutundikwa msalabani hatimaye alisema tena nimeshinda
akimaanisha binadamu hata kusumbuka kwa magonjwa, shida na
njaa”alisema mchungaji Msengi.
Mchungaji Msengi alisema kuwa yesu kristo
alikabidhi roho yake akimaanisha maovu yote na dhambi
zimekwisha kilichobaki ni binadamu kuendelea kutenda mema katika dunia.
Hata hivyo alisema kuwa binadamu wanatakiwa
kutafakari maneno ya mwisho ya mungu aliyonena kila binadamu anauwezo wa
kuililia familia yake kutokana na baadhi ya vitendo vya maudhi
vinavyoibuka na sio kumlilia aliyemkombozi wa wakristo yesu.
Wasiohudhuria katika ibada siku zote
na kutegemea siku maalumu kama za siku kuu alisema hao
wanatakiwa kuombewa na kuwatia moyo ili waweze kuhudhuria
wakati wote wa ibada, binadamu anatakiwa atende mema duniani
na kufuata yaliyonenwa na mwokozi yesu kristo ikiwa kuliombea taifa na familia
zao kwa ujumla.
0 Response to "JAMII IMETAKIWA KUJIOMBEA NA KULIOMBEA TAIFA HASA KIPINDI HIKI CHA MCHAKATO WA KUUNDA KATIBA MPYA."
Post a Comment