Habari za hivi Punde

JAMII YATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KUBAINI WAHAMIAJI HARAMU.





JAMII imetakiwa kutoa ushirikiano katika kuwabaini wahamiaji haramu ili waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi,hatua itakayosaidia kupata viongozi ambao ni wazalendo wenye uchungu na nchi yao badala  ya kuchagua mtu bila kujua historia yake matokeo yake uzalendo unakosekana.


Hayo yalibainishwa na Naibu Kamishina wa uhamiaji  wilaya ya shinyanga Salumu Farahani katika ofisi za uhamiaji mkoani shinyanga ambapo alisema kuwa kumekuwepo na wimbi la wahamiaji, ambao wamekuwa wakiishi nchini kinyume cha sheria na jamii kushindwa kuwafichua.
Kamishina huyo aliitaka jamii kuwabaini  wahamiaji haramu katika maeneo yao ili kuepusha madhara ya kupata viongozi ambao siyo wazalendo kwa kuwa na urai wa nchi nyingine, hali ambayo inaweza kuzorotesha maendeleo  ya Taifa.


“Changamoto tunazo kumbana nazo  katika kuwabaini wahamiaji haramu ni kukosekana kwa uwazi na ushirikiano kwa jamii, hii ni changamoto kubwa kwa kuwa wao ndiyo wanaishi nao lakini wanashindwa kuwa wazi,tunaiomba jamii itusaidie tukomeshe tatizo hili”alisema Kamishina huyo.

Pia aliongeza kuwa katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Sept 30 mwaka jana, walifanya msako na kukamata wahamiaji haramu 18 kwenye wilaya hiyo wengi wao wakiwa tayari wameshaweka makazi miaka mingi, hivyo kuwawia vigumu kuwarejesha katika nchi zao kwa kuwa hawatambuliki.

Hata hivyo Farahan alisema kutokana na changamoto hiyo,wameanza kuwaelimisha iliwapate vitambulisho vya urai na kuishi kwa mujibu wa sheria za nchi huku akisisitiza kuwa ushirikiano na uwazi ndiyo njia pekee  itakayosaidia kumaliza tatizo la watu kuhamia kutoka nchi nyingine na kuishi kinyemela.

Aliongeza kuwa,raia wa kigeni wengi wanaokamatwa ni kutoka Rwanda ndiyo inaongoza na kufuatiwa na Burundi pamoja na Uganda,ambapo wengi walikamatwa maeneo ya mjini wakati wakifanya shughulia zao.

0 Response to "JAMII YATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KUBAINI WAHAMIAJI HARAMU."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.