Habari za hivi Punde

TUME YA WATU 18 IMEUNDWA KUCHUNGUZA MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI



TUME  iliyoundwa ya watu kumi na nane na wenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama wakiwemo  mkuu wa mkoa wa shinyanga Ally Nasoro Rufunga na mkuu wa mkoa wa Tabora Fatuma Mwasa kuwa baini na kuwakamata watu waliohusika na mauaji ya watu watano katika mapigano ya wakulima na wafugaji yaliyotokea mpakani mwa mikoa hiyo miwili.

Mwenyekiti  wa  chama cha Mapinduzi  mkoani Shinyanga Khamis Mgeja  aliyasema hayo  kwenye kikao cha ndani cha CCM kilichofanyika wilayani Kishapu wakati wa ziara yake wilayani humo mara baada ya kusomewa taarifa ya mauji hayo na mkuu wa wilaya ya hiyo Wilson  Nkhambaku kuwa mapigano hayo yalitokea tarehe 29 marchi mwaka huu katika kijiji cha magogo wilayani kishapu mkoani shinyanga mpakani na wilaya ya Igunga mkoani Tabora na kusababisha mauaji wakati wakigombania Ardhi.


Mgeja alisema kutokana na tume hiyo ya uchunguzi kuundwa mda mrefu hivyo watu waliohusika na mauaji ya watu hao wanatakiwa kukamatwa haraka pamoja na kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili liwefundisho kwa watu wengine ambao hujichukulia sheria mkononi na kuchafua amani ya Nchi.

“Migogoro ya Ardhi hapa nchini inapaswa kukemewa kwa nguvu zote ikiwainavunja amani ya nchi na kudai kuwa hakuna kitu kibaya kana vita vya wenyewe kwa wenyewe ikiwa asilimia kuwa ya mapigano hayo watu hujuana udhaifu  wao na hivyo kulitia hasara taifa kwa kupoteza nguvu kazi na kupunguza pato la taifa”alisema Mgeja .

Hata hivyo  alisema kuwa moja ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi CCM nikuhakikisha watanzania wote wanaishi kwa mshikamano, amani , upendo na hakita kubali mtu yeyote kuvuruga amani ya nchi na kuitaka tume hiyo ya watu 18 ya mikoa yote miwili Tabora na Shinyanga kuhakikisha watu hao wanakamatwa ndani ya mwezi huu

Naye mkuu wa wilaya hiyo ya kishapu  wilson  Nkhambaku alisema  tume hiyo ya pande zote mbili zilikutana na kujadili walipofikia na kudai kuwa bado wanaendelea na uchunguzi huku akiwataja watu waliouawa katika mapigano hayo kuwani Peter Korongo Masolwa(72) Chawalwa Duke(50) Diblo Kingu(50) Mohamed msengi(40) na Kende Doma(70)

Nkhambaku pia almtaja mtu aliyejeruhiwa katika mapigano hayo kuwa ni Gilijisiji  Gilawida ambaye alijeruhiwa kwa kuchomwa mkuki na kudai kuwa hali yake inaendelea vizuri na kuongeza kuwa kamati ya ulinzi na usalama ya pande zote mbili bado zinaendelea na ulinzi wa eneo hilo la mgogoro pamoja na kutoa elimu kwa wafugaji na wakulima juu ya kudumisha amani

Kwa upande wake kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Shinyanga Kamishina Mwandamizi wa jeshi la polisi Evarist Mangala alisema mpaka hivi sasa hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa na Jeshi hilo kuhusuiana na mauaji ya watu hao watano yaliyo tokea katika mapigano ya Ardhi ikiwemo mto Manonga  baina ya wafugaji wa kishapu Mkoani Shinyanga  na wakulima wa Igunga Mkoani Tabor

0 Response to "TUME YA WATU 18 IMEUNDWA KUCHUNGUZA MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.