Alisema mbali na mapambano hayo halmashauri nyingi nchini suala la matumizi bora ya fedha za serikali bado halingatiwi, na kusababisha kuongezeka kwa rushwa kwa watumishi wake hasa wakuu wa idara ambao ndiyo wahusika wakuu katika matumizi ya fedha hizo.
Waziri Mkuchika alisema hayo jana wakati akiongea na wajumbe wa kikao cha ushauri cha Mkoa wa Simiyu (RCC) kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Barideco ulioko Mjini Bariadi, kikao kilichokuwa maalumu cha kupitisha bajeti ya mwaka 2014/15.
Alisema kuongezeka kwa rushwa katika halmashauri nyingi nyngi nchini, kunatokana na fedha nyingi zinazotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali kupitia moja kwa moja katika akaunti za halmshauri hizo.
Alibainisha ofisi ya Katibu Tawala Mkoa upata fedha chache ikilinganishwa na fedha zinazotolewa katika halmshauri, ambapo alieleza kuwa, wakuu wa idara, pamoja na wakurugenzi utumia nafasi hizo kujipatia fedha hizo kinyume cha utaratibu wa maadili ya kazi.
“ Kuwepo kwa uroho na tamaa ya mali baina ya watumishi hao wa serikali hasa katika ngazi ya halmashauri, huku wakiwa wanalipwa mishahara mikubwa kimekuwa chanzo cha kuongezeka kwa rushwa baina ya watumishi hao na kusahau kanuni za utumumishi bora”alisema .
Waziri huyo alileleza kuwa kuwepo kwa hali ya rushwa katika taasisi za serikali husababisha wananchi kukosa imani na serikali yao na kujichukulia sheria mikononi, kukosekana kwa huduma muhimu za kijamii, kutolewa kwa huduma duni,kuwa na viongozi wasio waadilifu pamoja na kupungua kwa pato la taifa hali inayosababisha kupungua kwa uwezo wa serikali katika kuwahudumia wananchi wake.
0 Response to "WAZIRI MKUCHIKA ASEMA RUSHWA KATIKA HALMASHAURI BADO NI KITENDAWILI"
Post a Comment