KITUO cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC) kimetoa
elimu ya Rasmu ya pili ya katiba kwa wananchi wa kata ya kitangili
mjini shinyanga ili wananchi hao wapate kuelewa pamoja na kujitokeza kupiga
kura pale Rasmu hiyo itakapo rudishwa mikononi mwa watanzania kama imekidhi
vigezo na maoni waliyoyapendekeza
Akitoa elimu kwa wakazi hao kwenye mkutano wa hadhara
mwanasheria wa Kituo hicho Jonsoni John alisema kuwa lengo la kutoa elimu
ya Rasmu ya pili ya katiba ni kukuza uelewa kwa watanzania iliwapate
kujua nini maana ya katiba hali ambayo itachangia kupata katiba safi ya
jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambayo itaongoza maisha ya watanzania na
vizazi vyake vyote.
John alisema baadhi ya watanzania hawaifahamu katiba ya nchi
hivyo wao kama kituo cha sheria na kutetea haki za binadamu wameona vyema
kutembelea baadhi ya mikoa hapa nchi kutoa elimu hiyo kwa wananchi pamoja
na kugawa vitabu na vipeperushi vinavyo elezea Rasmu ya pili ya katiba hali
ambayo itawapanua kimawazo na kutambua mambo gani ya muhimu yanafaa kuwepo
katika katiba mpya
Amesema Bunge
la Rasmu ya pili ya katiba lililopo mjini Dodoma ambalo hivi karibuni
litafanya kazi ya kupitia maoni ya watanzania pamoja na kufanya maboresho
yaliyopendekezwa juu ya kuundwa kwa katika mpya na Rasmu hiyo itakapo rudishwa
kwa watanzania ,itawakuta watanzania wanaupeo wa kutosha na hivyo kuichambua
kwa makini kama mapendekezo yao muhimu yamefanyiwa kazi.
Akizungumza kwenye mkutano huo mkurugenzi msaidizi wa
Kituo hicho Ezekiel Masanja amesema kuwa
Watanzania ndio wenye ridhaa ya kukubali ama kukataa Rasmu hiyo ya pili ya
katiba ipitishwe au isipitishwe na hivyokuamua kuendelea kutumia katiba ya
zamani ya mwaka 1977 endapo kama wakiona mapendekezo yao ya msingi hayapo
Katika mkutano huo wananchi walikuwa wanaulizwa
maswali juu ya Katiba na Rasmu ambapo asilimia kubwa walionekana kutokuwa na
uelewa wa vitu hivyo viwilli na mara baada ya kupewa elimu hiyo walifunguka
vichwa vyao na kuyatambua mambo muhimu yanayofaa kuwemo katika Rasmu ya pili ya
katiba ambayo ndio itaunda katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania
0 Response to "KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHATOA ELIMU YA RASMU YA PILI YA KATIBA."
Post a Comment