MAHAKAMA ya wialya ya Bariadi Mkoani Simiyu
imemuhukumu Mkazi wa mmoja liyejulikana kwa jina la Maganzo Zelamoshi mkazi wa
kijiji cha Zangho kata ya Mwabali wilayani humo, kifungo cha miaka 30 jela
baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na nyara za serikali bila ya kibali.
Akimsomea shtaka linalomkabili mtuhumiwa kabla ya
hukumu hiyo Mwendesha mashtaka wa TANAPA Eliasi Benjamini, alisema kuwa mnamo
tarehe 21 octoba 2013 mtuhumiwa alikutwa akiwa na pembe 2 za ndovu.
Alisema mtuhumiwa huyo alikutwa na pembe hizo mali ya
serikali bila ya kibali maalumu, ambapo alikamatwa na kufikisha mahakani, huku
mali hiyo ikiwa yenye dhamani ya shilingi Milioni 760.
Akitoa hukumu hakimu mkazi wa mahakama hiyo Robert
Oguda alisema mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa kutokana na ushaidi
uliotolewa na upande wa mashtaka na kuamuli kwenda jela kifungo cha miaka 30
pamoja na kulipa faini ya shilingi Milioni 17.
0 Response to " JELA MIAKA 30 KWA KUKUTWA NA PEMBE ZA NDOVU MBILI"
Post a Comment