WANAFUNZI 47 waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2013/14 katika shule za sekondari zilizopo manispaa ya Shinyanga hawajaripoti shule na kutojulikana walipo.
Hayo yalisemwa na ofisa elimu wa shule ya sekondari manispaa ya Shinyanga Daud Mkumbwa kwenye kikao kilichojumuisha viongozi wa sungusungu kutoka wilaya za manispaa,shinyanga na Kishapu kwaajili ya kujadili ajenda ya utoro mashuleni.
Mkubwa alisema kuwa kumekuwepo na wimbi la utoro mashuleni ikiwemo wanafunzi wa kike kupata mimba, kutohuduria masomo mara kwa mara ikiwa wanafunzi wakiume ni 21 na wakike 26 hawajaripoti shule mpaka sasa,ambapo aliwataka viongozi hao kushirikiana ili kuweza kuondoa changamoto hiyo.
“Manispaa ya Shinyanga inajumla ya shule 17 za sekondari idadi ya wanafunzi 2285, ikiwa mpaka sasa kunawanafunzi 2035 walioripoti wakiume ni 1013 na wakike ni 1022 ,ambapo wanafunzi 73 walibadilishiwa shule kwenda sekondari za binafsi”alisema Mkubwa.
Alisema kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wanafunzi kukaa shuleni kwa muda mfupi na baadaye kurudi nyumbani , ndoa za utotoni kuendelea kutokea huku wengine kupewa mimba hivyo jeshi la sungusungu wanatakiwa kufuatilia mienendo ya wanafunzi ili kubaini maendeleo yao kimasomo.
Naye katibu wa sungusungu tawi la Ikonongo Selemani Kanoni alisema kuwa watoto wa shule wanaopata mimba wamekuwa wakiwataja madreva wenye magari makubwa huku wazazi nao wakifanya siri jambao ambalo linakuwa ni vigumu kubaini waliowapatia mimba.
“Sisi sungusungu tutaendeleo kujitahidi kuwasaka na kuwakamata ila wazazi nao watoe ushirikinao, tatizo lililopo wanafunzi wengi wanaopewa mimba huwataja madreva wenye magari makubwa hivyo inashindikana kuwapata kiurahisi ili wafikishwe katika vyombo vya sheria huku baadhi ya wazazi wakimalizana na aliyempa mimba kinyemela”alisema.
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga alisema kuwa wanafunzi ambao wameshindwa kuripoti shule kwa sababu zisizo za msingi wazazi wao wahojiwe na kuchukuliwa hatua ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa kupitia viongozi wa vitongoji,vijiji na kata .
0 Response to "WANAFUNZI 47 WASHINDWA KURIPOTI KUANZA KIDATO CHA KWANZA."
Post a Comment