WATUMISHI wa idara ya mahakama mkoani Shinyanga
wametolewa hofu ya kuhakikisha wananchi wanashirikishwa ili kuweza kuboresha
miundombinu ya majengo kama wafanyavyo kwenye sekta zingine.
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga kwenye kilele cha
maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyka kwenye viwanja vya mahaka mkazi
wilaya nakuhusisha wadau kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo viongozi wa
madhehebu ya dini.
Rufunga amesema kuwa kumekuwepo na
miundombinu chakavu hasa kwenye mahakama za mwanzo pindi mvua ikinyesha
hasa msimu huu wa masika kesi zimekuwa zikiahirishwa hali hiyo inaendelea
kuwepo msongamano wa watuhumiwa magerezani kwa kuchelewa kwake.
Naye hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama
ya mkoa wa Shinyanga Rahimu Mushi alisema kuwa baadhi ya
mahakama za mwanzo miundombinu yake ni mibovu aliiomba serikali
kuwashirikisha wananchi kuboresha miundombinu hiyo kwa kuchangia kama
wanavyochangia kwenye sekta zingine.
Amesema hivi sasa mahakama imeongeza ufanisi wake katika
utendaji kazi kwa mwaka 2015 kulikuwa na mashauri 400 ya muda
mrefu lakini mpaka sasa kuna mashauri yasiyozidi 130 bado
kumekuwepo na changamoto ya baadhi ya wananchi kushindwa kujitokeza
mahakamani kutoa ushahidi kwa dhana kuwa watafungwa.
Naye mwakijilishi kutoka kwa
mawakili wa kujitegemea mkoani hapa Jacob Msomi alipokuwa akitoa taarifa yake
mbele ya mkuu wa mkao amesema kuwa tabia ya msemo kuwa polisi
ukienda ni bure nakutoka ni pesa hilo likomeshwe ikiwemo kukamata kamata hovyo
na kubambikia kesi ndio inayofanya hata magereza kuwepo msongamano.
|
0 Response to "WANANCHI KUCHANGIA UJENZI WA MAHAKAMA ZA MWANZO"
Post a Comment