WATU wadhanwao ni majangili katika pori la akiba Maswa waliofanya tukio la kutungua helkopita ya kampuni ya Mwimba Holding Limited na kusababisha kifo cha Rubani, Rodgers Charvis raia wa Uingeleza ambaye alikuwa akitekelezamajikumu yake jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata wahusika 9 pamoja na bunduki 29 ikiwemo meno ya tembo matatu.
Akiongea jana na waandishi wa habari mkoani Simiyu, Kamanda wa polisi mkoani hapa Lazaro Mambosasa alisema kuwa jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 9 ambao walihusika na tukio la kuangusha helkopita pamoja na kusababisha kifo cha Rubani wa ndege hiyo.
Alisema kuwa jeshi la polisi lilifanyamsako mkali ambao ulisababisha kuwakamata watuhumiwa wawili ambao ni ShijaMjika (38) na Masasi Mandogo (48) ambao walifanikisha kukamatwa kwawatuhumiwa wengine saba waliohusika katika tukio hilo.
Alisema baada ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao wawili walitaja na kuonesha meno mawili ya tembo yenye kilogram 31aliyeuawa januari 29 mwaka huu ambayo walikuwa wameyaficha kwenye daraja katika kijijicha Itaba.
Alibainisha kuwa baada ya kukamatwa kwa watuhumiwahao wawili jeshi la polisi liliwahoji na kukiri kuhusika na tukio hilo nakumtaja ambaye alifyatua risasi kwenye helkopita ambaye ni Dotto Pangali (41) ambaye alikamatwaakitaka kujaribu kutoroka kuelekea mkoa wa Shinyanga.
Kamanda mambosasa alisema kuwa baada ya kukamatwakwa mtuhumiwa huyo alikiri kutungua helkopita hiyo kwa kutumia Bunduki yaReffle yenye namba 7209460 CAR Na 63229 ambapo inamilikiwa na Mange Balumambaye kwa sasa anashiliwa na jeshi la polisi .
Kamanda huyo alisema kuwa baada ya upekuzi wa kinakwenye mji wa Dotto Pangali kulipatikana na Bunduki aina ya Reflle yenye namba3478 CAR Na 458 ikiwa na risasi 6 inayomilikiwa na Nghomango Jilala ambaye amekimbia na anaendelea kutafutwa na jeshi hilo.
Alifafanua kuwa katika oparesheni hiyo piawalifanikiwa kukamata watuhumiwa wengine ambao ni Njile Gonga (28),Iddi Mashaka(49),Mwigulu Kanga (40),Mapolu Njige (50)wote wakai wa kijiji cha Sungu ,DottoHuya (45)mkazi wa kijiji cha Itaba pamoja na Mange Balum(47)mkazi wa kijiji cha Itaba wilayani Meatu.
“katikamsako huo tumefanikiwa kukamata bunduki 27 pamoja na Risasi 141 ambazozinawamiliki ambao wamekuwa wakizikodisha silaha hizo kwa majangili kwenda kuulia tembo katika hifadhi za taifa na tumekamata Shotgun 11 na risasi 44,Raflle 10 na risasi zake 105 pamoja na magobole 6 yakiwa na risasi 2”alisema. |
0 Response to "MENO YA TEMBO YAKAMATWA HUKU WATU TISA WAKISHIKILIWA NA JESHI LA POLISI"
Post a Comment