Habari za hivi Punde

MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA ATAKA WANANCHI KUFAHAMU TARATIBU NA SHERIA DHIDI YA VYOMBO VYENYE DHAMANA


MKUU wa wilaya ya Shinyanga  Josephine Matiro  ametoa wito kwa wananchi  kushiriki utolewaji wa elimu  katika vyombo vinavyosimamia haki na sheria  ili kuweza kujua pindi haki inapotendeka nakuondoa manung’uniko yanayotokea mara kwa mara katika vyombo hivyo.

Hayo yalisemwa jana  na mkuu huyo wakati wa uzinduzi wa  maadhimisho ya wiki ya sheria  yaliyofanyika katika viwanja vya zima moto vilivyopo manispaa ya Shinyanga huku wananchi  wakitakiwa kujitokeza kusikiliza elimu inayotolewa katika makundi ya takukuru,jeshi la polisi na mahakama.

KARENY. Powered by Blogger.