WAHITIMU wa
chuo kikuu huria tawi la Shinyanga ambao
baadhi ni watumishi wa umma wametakiwa kuitumia elimu
walioipata kwa kuondoa changamoto zilizopo kwenye jamii na kunyanyua uchumi.
Hayo
yalisemwa jana na afisa elimu
msingi manispaa ya Shinyanga Paul
Magubiki aliyekuwa mgeni rasmi katika
mahafari ya tano kwa tawi hilo
lililojumuisha wahitimu 126 kwa ngazi mbalimbali.
Magubiki
alisema kuwa anatambua kuwa baadhi ya
wahitimu katika kozi mbalimbali ni wafanyakazi wa serikali kwenye utumishi wa umma hivyo waitumie elimu hiyo kuisaidia jamii kuongeza uchumi ikiwemo
kutatua changamoto zinazo ihusu jamii.
“Taifa hili
litaweza kuinua uchumi wake kulingana na watu wake wanavyofanya kazi changamoto zilizopo zijaribu kupunguzwa kwa kutumia elimu
waliyonayo kwa utumishi uliotukuka,
kwani watumishi hao ndio
watekelezaji wa maisha ya kila siku kwenye jamii hilo linawezekana”alisema
Magubiki.
Alisema
elimu kupitia masafa ya mbali
yameweza kutoa elimu kwa watumishi kwa kuwafanya waendelee na kazi huku wakipata elimu,hata wasio watumishi waliombali na maeneo ya chuo
waliweza kunufaika na masomo
yanayotolewa hivyo hakuna budi kuitangaza elimu kwa njia ya masafa.
Naye
mkurugenzi wa tawi hilo Martha Kabate
alisema kuwa chuo hicho kwa mkoa
wa Shinyanga kilianza rasmi mwaka 2006
kikiwa na jumla ya wanafunzi 11 hadi kufikia mwaka 2015 wahitimu
wamefikia 126 hali inaonyesha mwamko wa
kupata elimu ya juu kwa njia hiyo umeanza kufanikiwa.
“Ukiangalia mwamko wa elimu ya juu
kwa njia ya masafa ya mbali umeanza kuonekana katika jamii kwani mwaka 2006 waliohitimu ni
wanafunzi 11 huku mwanamke akiwa mmoja ambapo mwaka 2015 wamehitimu
wanafunzi 126 huku wanaume wakiwa 72 na wanawake 54 ila bado
kunachangamoto ya uhaba wa viti na meza za kujisomea chuoni hapo”.alisema
Kabate.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa chuo hicho Eustadius
Mkulu akisoma risala kwa niaba ya wanachuo alisema kuwa mafanikio waliyoyapata ni mengi kwa kuweza
pia kumudu kwa kujisomea bila walimu kwa
kupitia njia za mitandao
Naye
Magayane Desidery ni mfanyakazi wa jeshi la wananchi aliyehitimu digirii ya
kwanza ya sheria alisema kuwa alishawishika kujiendeleza ili kuweza kutatua
changamoto mbalimbali za kijamii huku akiwashauri wafanyakazi wenzake kuweza
kujiendeleza.
|
0 Response to "WAHITIMU CHUO KIKUU HURIA WAMEELEZWA KUITUMIA ELIMU HIYO KWA MANUFAA YA UMMA"
Post a Comment