WAZEE mkoani
Shinyanga wameiomba serikali kuwapatia
mikopo yenye mashart nafuu ili waweze
kujinyanyua kiuchumi kutokana na kuishi
maisha yenye umasikini uliokithiri nakuwa tegemezi katika familia.
Wazee
hao waliyasema hayo katika kikao cha kuhamasisha vyombo vya
habari kuhusu masuala ya wazee kwa
waandishi wa habari kilichoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali inayoongozwa na wanawake
wenye taaluma ya kilimo na mazingira (Tawlae) inayojishughulisha na masuala ya wazee.
Wazee hao kupitia
kamati ya baraza la wazee waliomba
serikali kupatiwa mikopo yenye mashart
nafuu kwa wazee ili waweze kujikimu kimaisha.
Mmoja wa
wazee hao John Kikulwa kutoka kijiji cha
Ibingo kata ya Samuye alisema kuwa wazee
bado hawajapewa kipaumbele katika jamii asilimia kubwa wamekuwa walezi wa
familia huku wakiishi maisha duni
nakukosa mikopo.
Mwenyekiti
wa baraza la wazee halmashauri ya
wilaya ya Shinyanga Edward Lupimo alisema kuwa wazee wanaishi maisha ya kimasikini ambapo kwa hivi
sasa baadhi yao wamepata unafuu kwa
kupitia mlango wa mfuko wa hifadhi ya jamii (Tasaf) kupata msaada na kujiongezea kipato.
Afisa
maendeleo ya jamii wa halmashauri ya
wilaya ya Shinyanga Joram
Magana alitoa ushauri kwa wazee kuwa wanatakiwa kuunda vikundi vitakavyo
tambulika kwenye halmashauri ili waweze
kupatiwa mikopo.
“Lengo la
serikali ni kila mmoja kuishi maisha bora nanyi mtakapo unda vikundi inatakiwa
vitambulike ndipo muombe mikopo kwa kuanzisha miradi ya kikundi kama ufugaji au kilimo hapo hapo mkiiomba wataalamu waje kwenye vikundi hivyo
wawapatie elimu”alisema .
Naye katibu
wa taasisi ya Tawlae Hellen Maleza
alisema kuwa wanaishukuru tasaf kwa kutoka msaada huo kwani hata baadhi ya
wazee walinufaika, pia wametakiwa kupokea ushauri wa kuanzisha vikundi
nakuvisajiri ili waweze kutambulika kwenye halmashauri.
0 Response to "WAZEE MKOANI SHINYANGA WAOMBA MIKOPO YENYE MASHART NAFUU"
Post a Comment