Habari za hivi Punde

MFUMODUME WAWA KIKWAZO KWA WANAWAKE KUKUZA UCHUMI

WANAWAKE  nchini wameelzwa kuwa mfumo dume ndio unaowakwamisha kuweza kupata mikopo katika taasisi za fedha kwa kukosa dhamana
 
Licha ya kuwa waaminifu zaidi kuliko wanaume wamekuwa kwakipata vikwazo mbalimbali vyakushindwa kuendesha biashara`zao na pindi  wanapohitajika kutoa dhamana kwaajili ya mikopo wengi wao hushindwa sababu ya  mfumodume
uliojengeka.
Hayo yamesemwa  janana meneja  wa benki ya CRDB tawi la Shinyanga  Said Pamui  katika semina ya uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake kupitia ukuzaji wa biashara iliyoandaliwa na benki hiyo.

Pamui amesema  biashara nyingi walizofungua wanawake  ni kama saluni,ufugaji wa kuku,duka na mama lishe  ambazo wameajiri vijana  wengi  nakuwapatia ajira ila bado wanachangamoto ya ukuzaji wa biashara zao hivyo wanatakiwa kujiamini kutumia fursa za taasisi za fedha kukopa nakujikwamua kiuchumi.

Pia amesema kuwa wanawake wamekuwa wakikutana na changamoto  zisizo za kifedha  ikiwemo masuala ya sheria  na taratibu  za kitaasisi,ukosefu wa elimu ya kibiashara  na fedha ,mazingira duni ya kufanyia biashara  na mitazamo hasi ya kiutendaji kwa mwanamke.
Naye mkuu wa wilaya ya Shinyanga  Josephine Matiro  aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa semina hiyo amewataka wanawake kubadilika kutumia fursa ya mkopo wa  akaunti ya malkia kwa wanawake  ulioanzishwa rasmi katika benki hiyo ili kuweza kujinyanyua kiuchumi.
Pia amewashauri  wanawake waunde vikundi nakuweza kuzipata shilingi million 50 zilizoahidiwa kutolewa na  Mheshimiwa Rais John Magufuli  fedha hizo zitatolewa ili zikopeshwe  na kuweza kufanya  biashara kwani mtu  hataruhusiwa kuchukua kama hutakuwa na biashara yoyote.
Baadhi ya wanawake waliohudhuria semina hiyo Josephine  Mwita ambaye ni mmiliki wa hoteli  ya Karena na Christina James mjasiriamali wa kutengeneza sabuni wamesema kuwa wako tayari kutumia mkopo wa wanawake katika benki hiyo huku wakiwataka wanawake wenzao kushirikiana kwa pamoja nakuunda vikundi.




0 Response to "MFUMODUME WAWA KIKWAZO KWA WANAWAKE KUKUZA UCHUMI"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.