Habari za hivi Punde

JESHI LA JADI LAPEWA DHAMANA YA KUSIMAMIA MICHANGO YA MRADI WA MAJI



WANANCHI  wa vijiji viwili  vya Mwamalili na Seseko kata ya mwamalili wilayani Shinyanga  wamekabidhiwa  kwa Jeshi la jadi sungusungu ilikukamilisha michango ya mradi wa maji utakao sambaza maji safi na salama katika vijiji hivyo  ambao unatoka ziwa Victoria kupitia tenki la maji (Shuwasa) .

Akilikabidhi Jeshi hilo la jadi kwa wanakijiji hao  mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga wakati akizindua mradi wa maji safi na salama katika vijiji hivyo viwili alisema kutokana na wanakijiji kukaidi agizo la serikali la sera ya maji ya  mwaka 2002, ambayo inasema kila mwananchi anapaswa kuchangia fedha katika miradi hiyo ya maji kuwa hanabudi kutumia mamlaka yake


Rufunga alimwambia kamanda wa Jeshi la jadi wa vijiji hivyo Charlse Makelesia washilikiane  na kamati ya maji ya vijiji hivyo viwili mwamalili na Seseko kuwa watumie  njia yeyote ile, ilikufanikisha michango ya mradi huo wa maji kwa wanakijiji hao, na ifikapo tarehe 30 mwezi huu michango yote iweimekamilika

Alisema enzi za mwalimu Nyerere wananchi walikuwa kipaumbele kuchangia miradi ya maendeleo, na baadhi yao ambao walikuwa wanakwamisha miradi hiyo jeshi la jadi sungusungu lilikuwa likipewa jukumu la kuwashughulikia ,kwa kuwakamatia mifugo yao au thamani yeyote ile,kwa lengo la kakamilisha michango  na kusukuma gurudumu la maendeleo

Rufuga alisema kutokana na mfumo huo aliokuwa akiutumia mwalimu Nyerere ambaye pia alikuwa Rais wa kwanza nchini Tanzania katika kufanikisha maendeleo kwa wananchi na kuinua uchumi wa taifa ,hivyo nayeye hanabudi kutumia mbinu hiyo katika kuleta maendeleo mkoani shinyanga

Akisoma Taaarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji katika vijiji hivyo viwili Afisa mtendaji wa kata ya mwamalili Simoni Mpaname alisema ujenzi huo wa mradi wa maji safi na salama ulitiwa saini tarehe 5 Agousti na utekelezaji wake ulianza tarehe 12 septemba mwaka jana ambapo kufikia tarehe 31 march mwaka huu, ulitakiwa kukamilika na kughalimu shilingi milioni 538,178,200

Mpaname alifafanua katika kijiji cha mwamalili wananchi walitakiwa kuchangia mradi huo kiasi cha fedha shilingi milioni 16.9 sawa na asilimia 2.5 katika kaya 501 ambapo kila kaya ilitakiwa kutoa fedha shilingi 35,000, na kudai kuwa hadi sasa wamechangia laki 469,900 na kubakiwa na deni la kukamilisha michango hiyo shilingi milioni 16,5.

Alisema  katika kijiji cha Seseko wananchi walitakiwa kuchangia Shilingi milioni 9 kwa kaya 360 ambapo kila kaya ilitakiwa kutoa fedha shilingi 30,000 na kudaiwa kuwa hadi sasa wamechangia laki 865,000 huku wakibakiwa na deni la kukamilisha michango hiyo shilingi 8,135,000 hali ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha mradi huo wa maji safi na salama katika vijiji hivyo viwili.

Akielezea sababu za wananchi kushindwa kuchangia fedha hizo mwenyekiti wa kamati ya maji katika vijiji hivyo Elisha Mahalala alisema sababu kubwa ni wananchi kuchanganya masuala ya maendeleo na siasa, kuwa Mmbuge wa jimbo la shinyanga Steven Masele aliwaahidi kuwaletea maji, hivyo hawawezi kutoa fedha hizo huku  baadhi yao wakisingizia wanakabiliwa na njaa.


0 Response to "JESHI LA JADI LAPEWA DHAMANA YA KUSIMAMIA MICHANGO YA MRADI WA MAJI"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.