Habari za hivi Punde

ASUSIA KUISHI KWA KUJINYONGA HUKU AKIACHA UJUMBE MZITO- CHALINZE

ASUSIA KUISHI KWA KUJINYONGA HUKU AKIACHA UJUMBE MZITO- CHALINZE
Mwanamme mmoja ambaye hakujulikana jina, amekutwa akiwa amejinyonga ndani ya kibanda shambani huku akiwa na karatasi iliyoandikwa ujumbe “Nawaachia dunia yenu muishi miaka 110”.  Mwenyekiti wa Kijiji cha Kibiki, Ally Hussein alisema  mwanamume  huyo amekutwa saa mbili usiku akiwa amefariki na hivyo kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Chalinze. Alisema askari walifika na kuukuta mwili wa marehemu ukiwa umefungwa kamba ya katani na alipopekuliwa alikutwa...

NI KWELI MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YANAWEZA KUTOWEKA KUFIKIA MWAKA 2030?

NI KWELI MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YANAWEZA KUTOWEKA KUFIKIA MWAKA 2030?
DAWA  ZITASAIDIA KUONDOA CHANGAMOTO YA MAAMBUKIZI? IMEELEZWA kwamba ifikapo mwaka 2030, kuna uwezekano mkubwa wa kudhibitiwa kwa  Janga la Ukimwi duniani,hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Umoja wa mataifa la kupambana na Ukimwi. Shirika hilo linasema idadi ya maambukizi mapya na wanaokufa kutokana na Ukimwi imeendelea kushuka. Hata hivyo jitihada zaidi za kimataifa zinahitajika kwani zilizopo hazitoshi kumaliza janga hilo. shirika la misaada la Medecins...

WANAJESHI WAAHIDI KUWEKA ULINZI KITUO CHA KULELEA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI.

WANAJESHI WAAHIDI  KUWEKA ULINZI  KITUO CHA  KULELEA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI.
Wanajeshi  wa kikosi cha 516 kambi ya kizumbi wakifanya usafi wa mazingira katika kituo cha Buhangija kinacholea watoto wasioona,walemavu wa viungo,wasiosikia na Albino. Sehemu ya misaada iliyotolewa na kikosi cha 516 kambi ya Kizumbi. Watoto wenye ulemavu wa ngozi Albino wakiwa katika eneo la kituo chao wanapolelewa. Misaada iliyotolewa na kikosi hicho ni pamoja na kilo 50 za sukari,mafuta ya kupaka cartoni mbili,ndoo mbili za mafuta ya kupikia,kilo 25 za unga wa sembe...

CHANZO CHA KUKITHIRI KWA MAUAJI YA VIKONGWE CHABAINISHWA

CHANZO CHA KUKITHIRI KWA MAUAJI YA VIKONGWE   CHABAINISHWA
MKUU wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya.      KUSHAMIRI  kwa matukio hayo ya mauaji kwa kukatwa mapanga kwa akina mama katika mkoa wa  Shinyanga kwa asilimia kubwa kunasababishwa na viongozi wa serikali za vijiji ambao hukosa uzalendo kutokana na  kugeuza matukio hayo kuwa vyanzo vya mapato yao kwa kuwahifadhi watuhumiwa wa vifo hivyo ambavyo hudaiwa husababishwa na imani za kishirikina.. Mkuu huyo wa wilaya, aliwashutumu viongozi wa...

ULEVI WAMPONZA BABA,MTOTO AANZA KUMCHARANGA KWA MAPANGA KWA KUCHOSHWA NA UNYWAJI WAKE

ULEVI WAMPONZA BABA,MTOTO AANZA KUMCHARANGA KWA MAPANGA KWA KUCHOSHWA NA UNYWAJI WAKE
MKAZI wa kijiji cha Ndala, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Andondile Mwasamlagila (50) amenusulika kufa baada ya kucharangwa na mapanga na mtoto wake, Yuda Mwasamlagila kutokana na ulevi wa kupindukia. Wakizungumza na blog hii, wanafamilia walisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 11 mwaka huu majira ya jioni ambapo mzee huyo akiwa amejituliza katika makazi yake, akivamiwa na kushambuliwa na mapanga na mtoto huyo. Walidai kuwa walisikia kelele za kuomba msaada kutoka kwa...

YULE ASKOFU (MBABE WA IMANI) ALIYEBURUZWA MAHAKAMANI NA WAUMINI WAKE SHINYANGA ASHINDWA KESI

YULE ASKOFU (MBABE WA IMANI) ALIYEBURUZWA MAHAKAMANI NA WAUMINI WAKE SHINYANGA ASHINDWA KESI
Waumini wa kanisa la EAGT Majengo manispaa ya Shinyanga wakimshangilia mchungaji wao David Mabushi baada ya kushinda kesi ndogo kupinga kuvuliwa uongozi wake ndani ya kanisa hilo.Kesi hiyo ilifunguliwa na waumini wa kanisa hilo wakishirikiana na mchungaji huyo dhidi ya kumpinga askofu wa kanda ya magharibi Rafael Machimu ambaye aliwafukuza wachungaji wanane na kulaumiwa na waumini ambapo kesi hiyo iliendeshwa mahakama ya wilaya shinyanga chini ya hakimu Thomson Mtani ikiwa kesi ndogo...

MWILI WA MTOTO ALIYEBAKWA NA KUUAWA KINYAMA -SHINYANGA WAZIKWA

MWILI WA MTOTO ALIYEBAKWA NA KUUAWA KINYAMA -SHINYANGA WAZIKWA
Mazishi ya mwanafunzi aliyeuawa kikatili kwa kubakwa kisha kutobolewa macho na watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa kichakani katika kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga yamefanyika katika makaburi ya familia katika kijiji cha Negezi kata ya Mwawaza katika manispaa ya Shinyanga. Mwanafunzi huyo  aliyekuwa anasoma darasa la tatu katika shule ya Msingi Negezi iliyopo kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga alikutwa ameuawa kwa kubakwa kisha kutobolewa...

KUNDI LA PANYA LAMSHAMBULIA MTOTO WA MWEZI MMOJA VIUNGO VYAKE VYA MWILI.

KUNDI LA PANYA  LAMSHAMBULIA MTOTO WA MWEZI MMOJA  VIUNGO VYAKE VYA MWILI.
Taarifa kutoka mjini Johannesburg Afrika Kusini zinasema - kuwa panya walimng'ata mtoto wa mwezi mmoja vidole na pua . Mtoto huyo anasubiri kufanyia upasuaji wa kuumba maumbile yake ya usoni baada ya tukio hilo huko Alexandra, Johannesburg . var obj0=document.getElementById("adsmiddle18173069026165791729"); var obj1=document.getElementById("adsmiddle28173069026165791729"); var s=obj1.innerHTML; var r=s.search(/\x3C!-- adsense --\x3E/igm); if(r>0) {obj0.innerHTML=s.substr(0,r);obj1.innerHTML=s.substr(r+16);} var...

KIKONGWE AUWAWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA, ACHARAZWA MAPANGA.

KIKONGWE AUWAWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA, ACHARAZWA  MAPANGA.
Kikongwe mwenye umri wa miaka 62 Raheli Jilungu mkazi wa kijiji cha Mishepu katika halmashauri ya wilaya ya  Shinyanga aliuawa kwa kukatwa shingo na mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina la Maganga Fuja akiwa na wenzake watatu .Chanzo cha mauaji hayo ni imani potofu za  kishirikina.  Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga  Justus Kamugisha atoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga kupambana na vitendo vya mauaji ya vikongwe.Kamugisha alisema kazi...

RACHAL MASHISHANGA AUKWAA UENYEKITI BAWACHA MKOA WA SHINYANGA CHADEMA

RACHAL MASHISHANGA  AUKWAA UENYEKITI BAWACHA  MKOA WA SHINYANGA CHADEMA
HUYU HAPA NI RACHAL MASHISHANGA  MBUNGE VITI MAALUMU CHADEMA MKOANI SHINYANGA AMEUKWAA UENYEKITI WA BAWACHA  CHADEMA MKOA.CHAMA  Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA),mkoani Shinyanga hatimaye kimepata viongozi wapya wa mkoa ,ikiwa imepita miaka mitatu bila ya kuwa na mwenyekiti wa mkoa wa Chama hicho ikiwa  wamemchagua  Peter Frank kuwa mwenyekiti kushika nafasi ya aliyekuwa  mwenyekiti  phlipo Shelembi aliyefariki  dunia mwaka 2011. var...

MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU,ABAKWA,ATOBOLEWA MACHO NA KUUWAWA.

MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU,ABAKWA,ATOBOLEWA MACHO NA KUUWAWA.
Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE MWANAFUNZI wa darasa la tatu  katika shule ya msingi Negezi iliyopo kata ya Ndala aliyefahamika kwa jina la Happy Kashidye (9), Mkazi wa Kata hiyo Manispaa ya Shinyanga siku ya jumapili  tarehe 24 ,aliuawa na watu wasio julikana  kisha  kumfanyia kitendo cha kumbaka na  kumtoboa...

WAUMINI WA KANISA LA EAGT WAANDAMANA KUMKATAA ASKOFU WA KANISA HILO.

WAUMINI WA KANISA LA EAGT  WAANDAMANA KUMKATAA ASKOFU WA KANISA HILO.
ASKOFU  wa kanisa  la EAGT kanda ya magharibi Rafael  Machimu  amefikishwa mahakamani  na waumini wa kanisa hilo kwa kitendo cha  kumpinga  kumfukuza  mchungaji wao  David Mabushi  bila kutenda kosa lolote jambo ambalo walilieleza ni  kwenda  kinyume na taratibu. Waumini hao wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari walisema wameamua kumfikisha mahakamani Askofu huyo wakipinga kitendo cha  mchungaji wao na...

WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI WAONGEZEKA KWA KASI KITUO CHA BUHANGIJA KWA HOFU.

WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI  WAONGEZEKA KWA KASI KITUO CHA BUHANGIJA KWA HOFU.
Meya  wa manispaa ya Shinyanga  Gullamu Hafidh Mkadamu akiwa meza kuu na   msimamizi ambaye ni mwalimu Peter Ajali wa shule hiyo akikabishiwa fimbo nyeupe 11 za watoto wasioona huku akielezwa wimbi la kuongezeka kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi kila siku watoto watatu mpaka wanne. MKAMA SHAKENGWA  NI KIONGOZI KATIKA KITUO CHA KULELEA WATOTO WENYE  ULEMAVU MBALIMBALI CHA BUHANGIJA   WAKIWEMO ALBINO.  WATOTO wenye ulemavu  wa ngozi ...

SHIDA YA MAJI WATOTO WASHINDISHWA KWENYE VISIMA,WAZAZI WASAKA MAJI NYAKATI ZA USIKU.

SHIDA YA MAJI WATOTO WASHINDISHWA  KWENYE VISIMA,WAZAZI WASAKA MAJI NYAKATI ZA USIKU.
WAKAZI wa kitongoji cha Mwabagikulu katika Kjiji cha  Ikonongo kata ya Salawe halmashauri ya wilaya ya Shinyanga  wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji hali ambayo inawafanya wakazi wa kijiji hicho  kuamka   nyakati za usiku kutafuta maji huku wakiwa na hofu ya kuhatarisha maisha yao,ambapo mkazi mmoja wa kijiji hicho Ndelemo Maguta alisema kuwa inawalazimu kutafuta maji nyakati za usiku  sababu ukienda majira ya mchana hakuna maji  huku watu ni wengi,wengine...

WATUHUMIWA SABA WA MAUAJI YA ALBINO WAKAWAMATWA BARIADI AKIWEMO MGANGA WA KIENYEJI.

WATUHUMIWA SABA WA MAUAJI YA ALBINO WAKAWAMATWA BARIADI AKIWEMO MGANGA WA  KIENYEJI.
Mkuu wa wilaya ya Bariadi  Erato Sima ambaye ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama wilayani humo. JESHI la polisi mkoani Simiyu limefanikiwa kuwakamata watu saba wanaodhaniwa  kuwa wauwaji wa aliyekuwa mlemavu  wa ngozi (albino) Munghu Mugata (40) aliyeuwawa kwa kukatwa mapanga  mnamo mwezi mei huko katika  kijiji cha Gasuma kata mwaubingi wilayani  bariadi. Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Kudawa Yelema (52) ambaye ni mganga wa jadi, Sitta Maduhu (39), Jasamila...

MAKAMPUNI YA UNUNUZI WA ZAO LA PAMBA YAONJA JOTO YA JIWE SOKO LA DUNIA.

MAKAMPUNI YA UNUNUZI WA ZAO LA PAMBA YAONJA JOTO YA JIWE SOKO LA DUNIA.
BAADHI ya makampuni ya ununuzi wa zao la pamba mkoani Shinyanga  yameonesha kujitoa kuendelea na ununuzi huo kwa kudai kuwa soko la dunia limeshuka  hawatapata faida ambapo chama kikuu cha ushirika  mkoani humo( Shirecu) kimeendelea na ununuzi  huo na kufikia kilo millioni 4.8 ikiwa lengo lake kwa mwaka huu ni kufikia kilo zaidi ya  millioni 8. Mojawapo ya kampuni lililojitoa na ununuzi huo ni kampuni ya Ahamu kwa kuona itapata hasara ambapo  asilimia...

CHANGAMOTO YA KUKOSA SOKO LA UHAKIKA KWA WAKULIMA CHANZO CHA UMASIKINI.

CHANGAMOTO YA KUKOSA SOKO LA UHAKIKA KWA WAKULIMA CHANZO CHA UMASIKINI.
WAKULIMA WAKIWA SHMABANI WAKIVUNA ZAO LA DENGU KATIKA KIJIJI  CHA AMANI KATA YA SALAWE HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA. WAKIBEBA ZAO LA DENGU NA KUPELEKA NYUMBANI KWA KUCHAMBUA. WAKULIMA  wa zao la dengu katika kijiji cha  Amani kata ya Salawe halmashauri ya wilaya ya  Shinyanga  bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa  soko la uhakika  kwenye  zao hilo ikiwemo miundombinu ya barabara kuwa mibovu hali ambayo inawafanya kushindwa...

WIZI WA NYAYA ZA SIMU WASABABISHA HASARA YA ZAIDI YA SHILINGI MILLIONI 133 MANISPAA YA SHINYANGA.

WIZI WA NYAYA ZA  SIMU WASABABISHA HASARA YA ZAIDI YA SHILINGI MILLIONI 133 MANISPAA YA SHINYANGA.
BAADHI ya wananchi manispaa ya Shinyanga  wametakiwa kuwapatia elimu zaidi  vijana  na kuondoakana na uhalifu ambao chanzo chake ni utumiaji wa  madawa ya kulevya, biashara ya vyuma chakavu ikiwemo wizi wa  nyaya za simu hali ambayo imefanya shirika la mawasiliano  ya umma nchini TTCL kwa wilaya  shinyanga kupata hasara ya zaidi ya shilingi million 133. var obj0=document.getElementById("adsmiddle15420993657888990177"); var obj1=document.getElementById("adsmiddle25420993657888990177"); var...

MBWA AMTAFUNA MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU NA KUPOTEZA MAISHA

MBWA AMTAFUNA  MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU  NA KUPOTEZA MAISHA
Moja ya mbwa anayedaiwa kumla mtoto Ibrahim Faraja Chipungahelo (9) akiwa ameuawa pia. MWANAFUNZI wa Shule ya Msingi Ludewa mkoani Njombe, Ibrahim Faraja Chipungahelo (9) ameuawa kikatili na mbwa wanaosadikiwa kuwa na kichaa kisha kuliwa nyama.  Tukio hilo lililoacha simanzi kubwa kwa wakazi wa Ludewa mjini lilijiri saa 7 mchana wa Agosti 8, mwaka huu katika eneo la Ikilu ambapo marehemu na wenzake walikuwa wakipita nje ya nyumba ya mtu aliyejulikana kwa jina...
KARENY. Powered by Blogger.