Habari za hivi Punde

WAFYATULIANA RISASI WAKIWA MAHAKAMANI SABABU YA KUTOFAUTIANA KIMAWAZO.

Visa vya ufyatulianaji wa risasi mahakamani nchini Afrika Kusini vimekuwa vikiongezeka


Wafungwa wawili wamepigwa risasi walipokuwa wakijaribu kutoroka kutoka katika mahakama moja nchini Afrika Kusini.
Afisa mmoja kutoka wizara ya sheria aliambia chama cha wanahabari nchini humo kwamba wafungwa waliokuwa wanasubiri kusikilizwa kwa kesi yao waliokota silaha kutoka kwenye jaa la taka.
Inaarifiwa wafungwa hao walianza kufyatuliana risasi na maafisa wa polisi.
Tukio hilo lilitokea katika mahakama kuu mtaa wa Mthatha katika mkoa wa Eastern Cape.
Mthunzi Mhaga, ambaye ni waziri wa sheria, alisema kuwa mfungwa mmoja alijeruhiwa mguuni wakati wa ufyatulianaji risasi.
''Walijaribu kutoroka walipoingia ndani ya majengo ya mahakama , '' alisema bwana Mhaga.
''Baada ya kuipata bunduki, walianza kufyatuliana risasi na maafisa wa polisi, '' aliongeza kusema bwana Mhaga.
Alisema kuwa polisi waliweza kudhibiti hali.
Kufuatia visa vya hivi karibuni vya ufyatulianaji risasi mahakamani mjini Pretoria na Cape Town, waziri wa sheria alisema kuwa atahakikisha uwepo wa sheria z akudhibiti ulinzi katika majengo ya mahakama

0 Response to "WAFYATULIANA RISASI WAKIWA MAHAKAMANI SABABU YA KUTOFAUTIANA KIMAWAZO."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.