Habari za hivi Punde

HALMASHAURI KANDA YA ZIWA WATAKIWA KUWEKA AKIBA YA ARDHI KATIKA MAENEO YAO

HALMASHAURI KANDA YA ZIWA WATAKIWA KUWEKA AKIBA YA ARDHI KATIKA MAENEO YAO


HALMASHAURI  za kanda ya ziwa zimetakiwa kuwa na akiba ya Ardhi ilikuweza kutoa fursa kwa wawekezaji pindi wanapokuja kuwekeza katika maeneo yao ikiwa changamoto kubwa imebainika kukosa  maeneo ya kuwekeza  pindi  yanapohitajika  ili kuweza kunyanyua uchumi .

ajinyonga

ajinyonga


MTU mmoja aliyejulikana kwa jina la Shija Mfuko (60) mkazi wa kijiji cha Zobogo kata ya Itwangi tarafa ya Itwangi wilaya ya Shinyanga amekutwa amekufa kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani katika shamba la mapera lililopo mpakani mwa kijiji hicho na kijiji jirani cha Nhumbili kata ya Tinde wilayani humo.

mafunzo habari za uchunguzi za biashara mwanza

baadhi ya wanafunzi wa chuo cha SAUTI Mwanza wakifuatilia mafunzo ya habari za uchunguzi za biashara

KIKONGWE AJINYONGA KWENYE SHAMBA LA MAPERA

KIKONGWE AJINYONGA KWENYE SHAMBA LA MAPERA
MTU mmoja aliyejulikana kwa jina la Shija Mfuko (60) mkazi wa kijiji cha Zobogo kata ya Itwangi tarafa ya Itwangi wilaya ya Shinyanga amekutwa amekufa kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani katika shamba la mapera lililopo mpakani mwa kijiji hicho na kijiji jirani cha Nhumbili kata ya Tinde wilayani humo
Wananchi walioshuhudia tukio hilo walisema walimkuta mzee huyo amejinyonga kwenye shamba la mapera jana Jumatano majira ya saa 11 jioni huku wakidai kuwa huenda kifo hicho kimetokana na kuchanganyikiwa kwa mzee huyo baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mashuhuda hao waliongeza kuwa siku hiyo ya Jumatano marehemu aliaga muda wa asubuhi kuwa anaenda kufanya mazoezi kutokana na kwamba alikuwa amefanyiwa oparesheni ya tumbo lakini wakashangaa kwanini hakurudi mapema ndipo wakaanza kumtafuta na kumkuta amejionyonga kwenye shamba la mapera.
Akizungumza na mwandishi wa habari  mtoto wa marehemu aitwaye Shija Mathias alisema ni kweli baba yake alikuwa amefanyiwa oparesheni ya tumbo mwezi Juni mwaka huu,na tayari alikuwa amepona na kila siku amekuwa akifanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya kuimarisha afya yake.
"kifo hiki kinasikitisha sana na kimetushitua ,kwani mzee amekuwa akifanya mazoezi kama kawaida leo kaondoka asubuhi hakurudi tena hajarudi muda mrefu ndiyo tukaanza kumtafuta na polisi wameturuhusu kuuchukua mwili wa marehemu,na hapakuwa na mgogoro wowote hapa nyumbani",alisema Mathias.
Kwa upande wake afisa mtendaji wa kijiji cha Zobogo Elizabeth Gabriel alisema  kifo cha mzee Jondo huenda kimetokana na kuchanganyikiwa kwani alikuwa ameugua kwa muda mrefu na inasemekana kuwa kidonda cha oparesheni kilikuwa kinatoa maji maji.
“Kutokana na taarifa nilizozipata marehemu pia alitoroka siku moja kabla ya tukio alitoroka lakini ndugu zake   walifanikiwa kumpata mzee huyo akiwa amejinyoga.


KARENY. Powered by Blogger.