Habari za hivi Punde

IDARA YA UHAMIAJI WATUMISHI WAKE WAPIMA V.V.U KWA HIARI WAKIONGOZWA NA KATIBU TAWALA WILAYA YA SHINYANGA BONIFACE CHAMBI.


Kamanda uhamiji mkoa Anna maria Yondani akiwa kwenye zoezi la upimaji  v.v.u ambapo anasema ni moja ya mipango iliyojiwekea idara hiyo kupima watumishi wote pamoja na familia zao.


Kamanda wa uhamiaji mkoa  wa Shinynga  Annamaria Yondani akiwa katika zoezi la upimaji V.V.U  ambapo anasema kuwa  upimaji umekuwa ni jambo la kawaida hivyo jamii ione umuhimu wa kupima afya zao.Watumishi wa idara ya uhamiaji wakijiandaa zoezi la upimaji v.v.u mara baada ya kuhutubiwa na aliyekuwa mgeni rasmi katibu tawala wilaya Boniface Chambi.


Katibu tawala wilaya Boniface Chambi akipimwa V.V.U kwa hiari  baada ya kuongoza utumishi wa idara ya uhamiaji zoezi hilo wakiwemo wageni waalikwa kutoka idara mbalimbali ndani ya mkoa  wa Shinyanga.
Katibu tawala huyo wa wilaya ya Shinyanga alisisitiza jamii kupima na kuondokana na unyanyapaa kwa wale wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi na kujenga mazoea ya kupima kwa hiari sio ukimwi pekee hata kwenye magonjwa mengine kama vile kisukari na presha.

KARENY. Powered by Blogger.