Mkuu wa kituo cha polisi cha Nyamboge kilichopo katika kata ya Katoma wilayani Geita mkoani Geita amenusurika kupigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kukutwa akitaka kufanya mapenzi na mwanafunzi katika chumba anachoishi mwanafunzi huyo(Geto).
Akielezea
tukio hilo binti huyo (jina tunalo)(17) anayesoma kidato cha nne
alisema siku ya jumapili mkuu huyo wa kituo alituma maaskari wawili wiki
jana wakaenda kumkamata.
"
Hata sijui kosa langu,nilikamatwa nikalazimika kwenda na nilipofika
alianza kunilazimisha natembea na mwalimu wangu,nilipokataa nilianza
kupigwa na kulazimishwa kuandika maelezo",aliongeza mwanafunzi huyo.
Alisema
baada ya kukataa kuandika maelezo alipelekwa rokapu na muda mfupi
alifuatwa na askari mmoja kati ya wale waliomfuata anapoishi, alianza
kuandika maelezo na kulazimishwa kusaini.
Alisema
baada ya kugoma kuandika alipigwa sana na kuamua kusaini kutokana na
kutishiwa kufungwa na baada ya kusaini aliitwa na OCS huyo na kumwambia
aende nyumbani lakini arudi jioni ana shida naye ya muhimu sana lakini
hakurudi kutokana na kuchoka na kipigo alichokipata kituoni hapo.
"Kutokana
na mkuu huyo wa kituo kutuhumiwa na mwanafunzi kuwa anamtaka kimapenzi
ilibidi awaambie wanafunzi wenzake na wananchi na baada ya hapo
wakatengeneza mtego ili wamnase",walisema mashuhuda wa tukio hilo.
"Siku
ya jumapili jana mkuu huyo wa kituo alikwenda nyumbani kwa mwanafunzi
huyo na kuomba wafanye mapenzi kwa kuwa wenzake anaoishi nao hawakuwepo
lakini aligoma kufanya hiyo ",walisema mashuhuda wa tukio hilo
"Kutokana na mtego wa wananzengo,muda mfupi wananchi
waliokuwa wamemuona OCS anakwenda kwa binti huyo walifika hapo na
kufunga mlango kwa nje na kuanza kupiga mwano",waliongeza
Walisema
kufuatia hali hiyo OCS huyo alivunja mlango na kutoka nje huku
wanachi wakimkamta na kuanza kumpiga lakini aliokolewa na askari na kufikishwa katika kituo kikuu cha polisi cha wilaya ya Geita.
Hata hivyo baadhi ya wanakijiji waliokuwepo kwenye tukio hilo
walisema OCS huyo amekuwa na tabia mbaya sana kwa wanafunzi wanaosoma
katika shule hiyo kwa kuwatongoza na wakikataa anawasingizia kesi au
ndugu zao hivyo kuomba serikali kumchukulia hatua kali OCS huyo kwa
kitendo hicho kiovu.
Diwani wa kata hiyo Josephat Komanya alithibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kulaani vikali kitendo hicho na kuwaomba wanafunzi wa
kata hiyo kuendelea kuwataja viongozi ambao wanawataka kimapenzi kwa
nguvu.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoni hapa Joseph Konyo alipopigiwa sm yake ya
mkononi kuzungumzia juu ya tukio hilo alikata na alipotumiwa ujumbe
mfupi wa maneno zaidi ya mara mbili hakujibu.
Na Valence Robert- Geita
0 Response to "MKUU WA KITUO CHA POLISI CHA NYAMBOGE -MKOANI GEITA ANUSURIKA KIPIGO TOKA KWA WANANCHI"
Post a Comment