Baadhi ya wazazi na viongozi wa kijiji
Wananchi
wa Kijiji cha Maendeleo Kata ya Ruiwa wameiomba Serikali kuingilia kati hatma
ya shule ya Msingi ya Kijiji hicho kutokana na uhaba wa walimu na madarasa ya
kusomea.
Wakionge
na Mbeya yetu kwa masikitiko baadhi ya wazazi walisema uongozi wa Kijiji hicho
umeshindwa kuiendeleza shule hiyo licha ya kukusanya fedha kutoka kwa wananchi
na wafugaji Kijijini hapo.
Jason
Halinga mmoja wa wazee maarufu Kijijini hapo alisema kuwa yeye ana watoto sita
wanaosoma shuleni hapo wanaosoma darasa la kwanza hadi la sita wakifundishwa na
Mwalimu mmoja tu aliyefahamika kwa jina la Laiton Ngoli.
Mwalimu
huyo aliyeanza kufundisha mwaka 2007 hajawahi kulipwa mshahara wowote licha ya
kufundisha kila siku ingawa wazazi wamekuwa wakijitahidi kuchangia shilingi
elfu moja kwa kila mwanafunzi lakini wamekuwa wakilipa baadhi tu.
Mmoja
wa wafugaji aliyefahamika kwa jina la Kuzenza Mtogambuli alisema yeye amechangia
zaidi ya shlingi laki sita kwa ajili ya ununuzi wa mbao na mabati kwa madaasa
mawili yanayotumiwa na wanafunzi wa shule hiyo.
Kwa
upande wake Mwalimu Laiton Ngoli alisema kuwa mbali ya changamoto za madaasa
shule hiyo haina nyumba ya mwalimu wala maliwato na kufanya baadhi ya watoto
kujisaidi vichakani.
John
Kalikumoyo aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Ijumbi alisema kuwa shule
hiyo ilipata kibali cha kujengwa mwaka 2013 lakini fedha zilizochangwa na
wananchi hazionekani zilipo hali inayowakatisha tamaa wazazi.
Uchunguzi
umebaini shule hiyo ina zaidi ya watoto 320 wanaosoma kwa kubadilishana
madarasa hayo mawili na Mwalimu Ngoli anafundisha darasa la awali hadi darasa
la sita ingawa watoto wa darasa la nne na darasa la sita wamesajiliwa shule ya
msingi Ruiwa.
Kutoka
shule hiyo ya Maendeleo Ishungu watoto hutembea umbali wa kilometa zaidi ya
nane na hali inakuwa mbaya wakati wa masika ambapo watoto hushindwa kuhudhuria
masomo kutokana na mto Gwili kujaa maji.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Maendeleo Charles Mkisi alisema kuwa wameanza kuchimba msingi
kutokana na fedha zilizochangwa lakini changamoto kubwa ni ukosefu wa
ushikiano na Viongozi wa Kata ambapo wanakosa msaada wa usimamizi wa majengo
hayo ambapo wameishia kuchimba msingi tu.
Kwa
upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Regimius Ntimaya alisema kuwa
atafuatillia suala hilo.
Na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
0 Response to "MWALIMU AONJA MACHUNGU YA AJIRA YAKE,WANAFUNZI MBIONI KUPATA MLIPUKO WA MAGONJWA."
Post a Comment